Maajabu ya pyramid Misri

Maajabu ya pyramid Misri

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
PYRAMID linalopatikana Misri lilikua ndio jengo refu zaidi lililojengwa na mwanadamu miaka 4000 iliyopita .Mojawapo ya pyramid refu zaidi huko Misri (Egypt) lina urefu wa futi 481 sawa na jengo lenye ghorofa 48.Lina uzito wa tani million 14.5,limechukua eneo la mraba hekari 13 sawa na viwanja kumi vya mpira wa miguu.Inaaminika kua lilianza kujengwa mnamo 2540BC na kumalizika miaka 23 baadae.

PYRAMID kubwa zaidi MISRI (Egypt) lilitumia matofali (majabali,mawe) 2,300,0000 (million mbili na laki tatu) na inakadiriwa kua kila tofali/jabali/jiwe lilikua na uzito wa tani 7, kwenye kilele cha pyramid hilo jiwe lililotumika kufunika juu kabisa lina uzito wa tani 50 mpaka leo wazungu wanajiuliza ni kina nani walilipandisha jiwe hilo na ilifanyika vipi jiwe la namna hiyo kupandishwa juu urefu wa futi zaidi ya 400 na binadamu jambo ambalo ni gumu kulielewa

Pia unaambiwa PYRAMID hilo lilijengwa kwa vipimo vya hali ya juu na ustadi mkubwa sana jambo ambalo linathibitisha kua taaluma ya uhandisi na hesabu imeanza kutumika miaka mingi sana kipindi hicho wazungu bado wana ng'aa macho mapangoni

Pande zote tatu za PYRAMID zipo sawa na unaambiwa huwezi kuona kimvuli cha pyramidi hata ukae upande gani hii inamaana kua hata jua likae upande gani huezi kuona kimvuli cha pyramid hili,hesabu zilizotumika kujenga pyramid hilo ni pasua kichwa,

Wazungu walipokuja Africa hawakuchukua vibovu bali walichukua vitu vizuri vyote na kuhamishia kwao waliiba taaluma mbalimbali na kuzihamishia kwao na kuhakikisha wanapoteza ushahidi wa kua zilianzia afrika,kabla ya wazungu kuja Africa tulikua tumekamilika kwenye kila idara madaktari,wanajeshi,wabunifu wa kila aina wote hawa walikuja kuzolewa na kupelekwa utumwani kuwatumikia watu weupe walituachia majonzi na umasikini wakutosha ambao bado unatutesa mpaka leo
 
Pyramid zilijengwa na waafrika au walijenga waisraeli?
Pyramid zilijengwa na waisrael wakati walipokuwa utumwani Misri miaka miaka mingi iliyopita BC mi ndo nafahamu hvyo.
 
Inasemaje teknolojia ya zamani ya ujenzi ilikuwa kubwa kuliko saiv...Kuna mchambuzi mmoja alisema waliojenga majengo hayo na mengine zamani kuanzia mnara wa babeli na miji ya Mesopotamia etc wakifufuka leo wakute mnajenga majengo wataona Ni Kama mnachezea matope
 
Pyramid zilijengwa na waafrika au walijenga waisraeli?
Pyramid zilijengwa na waisrael wakati walipokuwa utumwani Misri miaka miaka mingi iliyopita BC mi ndo nafahamu hvyo.
Kwa mujibu wa mapokeo tuliopokea kutoka kwa wazungu waisrael walikuwa ni vibarua wakitumikishwa kazi mainjinia wenyewe walikuwa ni wamisri

Na kwa mujibu wa mapokeo hayohayo toka kwa wazungu waisrael waliingia misri pindi baada NABII YUSUPHU kushika hatamu ya uongozi

Na kwa mujibu ya mapokeo hayohayo tuliopokea kwa wazungu NABII YUSUPH wakati anaingia misri km mtumwa kwa ajiri ya kuuzwa

Wamisri tayari walikuwa wanawazika makuhani mafarao wao katika mapyramid !!!
 
PYRAMID linalopatikana Misri lilikua ndio jengo refu zaidi lililojengwa na mwanadamu miaka 4000 iliyopita .Mojawapo ya pyramid refu zaidi huko Misri (Egypt) lina urefu wa futi 481 sawa na jengo lenye ghorofa 48.Lina uzito wa tani million 14.5,limechukua eneo la mraba hekari 13 sawa na viwanja kumi vya mpira wa miguu.Inaaminika kua lilianza kujengwa mnamo 2540BC na kumalizika miaka 23 baadae.
Hotep......
Misri ya kale iliitwa Kemet, wazungu waliharibu pua za sanamu zilizopo Kemet ili ionekane kwamba sio kazi ya mtu mweusi
 
Pyramid zilijengwa na waafrika au walijenga waisraeli?
Pyramid zilijengwa na waisrael wakati walipokuwa utumwani Misri miaka miaka mingi iliyopita BC mi ndo nafahamu hvyo.

Kwanini unaamini walijenga waisrael na sio africans?
 
kuna lijinga limesema piramid walijengwa waisrael, guu ni ujinga na upumbv, maana hizo zmejengwa hata kabla hao waisrael wenu feki hawajakwenda uko misri, pia ktk historia dunia nzma hakuna utumwa wa muisrael nchin misri, zadi stor hizo unapata ktk biblia, biblia yenyewe imeshindwa kueleza ule utumwa ukikuwaje, yaan inajipinga yenyewe, anaebisha na abishee ila ukwel hakuna utumwa wa muisrarl misri, zaid ya propaganda kutengenezwa ili muafriak achukiwe, kama ujuavyo mafarao wote walkuwa watu weus, wamisri walkuwa weusi yaan waafrka, ayo majizi ya kiarabu yameamia juzi tuu baada ya dora kuangushwa kwa husda na wivu wa mtu mweupe, pyramid zile zlkuwa na kazi kubwa ma yakutisha, lkn wazungu wansema et pyramid ilkuwa kwaajil ya maziko kumbe ni zaid ya hayo, kuna shahdi nying sana, haya mambo kuyajadil unatakiwa usibase kwenye mahaba ya dini wala chuki zakininga, Afrika ndyo mama wa dunia na mjue tu kuwa mapyramid hayapo misri tu bal mpka sudani, sudan yako mengi kulko misri, lkn misri ndpo yapo makubwa kulko ya sudan,...kazi moja wapo ya pyramid ilkuwa ni kufungua mlango na kuingia ktk dimension ya pepo(mbingu) na hata ule mnara wa babel ulijengwa kwa stail ya pyramid na ulkuwa ni pyramid iliyojengwa hapa hapa afrika, mambo n meng muda mchache
FB_IMG_16235954192984232.jpg
 
kuna lijinga limesema piramid walijengwa waisrael, guu ni ujinga na upumbv, maana hizo zmejengwa hata kabla hao waisrael wenu feki hawajakwenda uko misri, pia ktk historia dunia nzma hakuna utumwa wa muisrael nchin misri, zadi stor hizo unapata ktk biblia, biblia yenyewe imeshindwa kueleza ule utumwa ukikuwaje, yaan inajipinga yenyewe, anaebisha na abishee ila ukwel hakuna utumwa wa muisrarl misri, zaid ya propaganda kutengenezwa ili muafriak achukiwe, kama ujuavyo mafarao wote walkuwa watu weus, wamisri walkuwa weusi yaan waafrka, ayo majizi ya kiarabu yameamia juzi tuu baada ya dora kuangushwa kwa husda na wivu wa mtu mweupe, pyramid zile zlkuwa na kazi kubwa ma yakutisha, lkn wazungu wansema et pyramid ilkuwa kwaajil ya maziko kumbe ni zaid ya hayo, kuna shahdi nying sana, haya mambo kuyajadil unatakiwa usibase kwenye mahaba ya dini wala chuki zakininga, Afrika ndyo mama wa dunia na mjue tu kuwa mapyramid hayapo misri tu bal mpka sudani, sudan yako mengi kulko misri, lkn misri ndpo yapo makubwa kulko ya sudan,...kazi moja wapo ya pyramid ilkuwa ni kufungua mlango na kuingia ktk dimension ya pepo(mbingu) na hata ule mnara wa babel ulijengwa kwa stail ya pyramid na ulkuwa ni pyramid iliyojengwa hapa hapa afrika, mambo n meng muda mchacheView attachment 1837942
Wala cjakataa kuwa m n mjinga ndo maana nikaamua kusema kile nachofahamu hapo kuna kitu nimejifunza ambacho nilkuwa cfahamu, usijerudia kumuita mtu mpumbavu kama hujamfundisha, huyo unaemuita mpumbavu akifundshika hawez kuwa mpumbv
 
Akili nyingi ilianzia Arabuni na Africa baadaye wazungu wakarupora
 
Back
Top Bottom