maajabu ya shule za kata....

We ushaambiwa kuna mkuu wa mkoa, mind you mkuu wa mkoa, Arusha huko, anakwepa kwenda kwenye mikutano kwa sababu hajui kiingereza.

Janga la kitaifa.

nakubaliana na wewe sisi wakati tunamaliza form six kuna mkuu wa mkoa alikuja kwenye graduation akaongea zaidi sa masaa matano. sasa ni akili hiyo?
 
Mh jaman inatia huruma kwa kwel,mtu anamaliza form four english mamamkwe,kujieleza f,math ndo usiseme.yote hii n kutokuwa na uongozi mzuri,sera mbov
 
Huyu mwanafunzi ana IQ nzuri tena sana,tatizo ni lugha tu!angeambiwa aandike kwa kiswahili angeeleweka vizuri tu.

mkuu, huyo mwanafunzi ana IQ ndogo sana, na nahisi hata kiswahili aligonga mswaki.
 

halafu eti wakipata zero wanazimia.... damn...
 
mbona kuna watu wapo vyuo vikuuu......hawajui kuongea kiingereza inawezekana huyo dogo ni mkali kwenye mathematics, phyiscs chemitry ......masomo ya kike hayo ya essay anaona yanampotezea muda
 
Yooo yoooo nahisi huyo kayumba ndio alishusha 16barz kwenye majibu
 

Halafu huyo huyo mwambie akuandikie bongo flava, atakuwekea na vionjo.
 
Sijui ndiyo mwanafunzi wako mkuu, lakini nachoweza kusema ni kuwa walimu wengi nao ni funika kombe mwanaharamu apite, kama wabunge vile. Tatizo hapo lipo wazi mtoto hajajisomea, hakuelewa lile somo na hajapata kitu, pamoja na kingeereza kuwa kibovu!!

kumbuka leo huyo ndiyo mawaziri wetu kesho.
hili balaa tulilonalo kwa tanzania ni kubwa. haliwezi kutatuliwa kirahisi hivyo. leo nimeona ktk TBC KIONGOZI anaulizwa kama watoto kukaa chini tena kwenye mchanga baada ya kuonyeshwa shule moja huko dar kinyelezi, majibu ni kwamba mwanafunzi hawezi kufeli kwa sababu ya kukaa chini.
 
Kingereza ndio kinawashinda na wakati mwalimu anafundisha na wanafunz wale ambao ni goigoi wanaachwa mbali sana.
 
Nachelea kumlaumu mwanafunzi huyu, ni wazi kwamba amejikuta hapo kutokana na sera yetu ya elimu. kama serikali inadhani kwamba kuna haja ya watoto wetu kuwa mahiri ktk lugha hii ya kiingereza, basi ni budi kubadilisha sera na kukifanya kiingereza kuwa lugha ya kufundishia from the very baby class. na kinyume chake iwe hivyo.
Hao tunaowaona wanajieleza vizuri kwenye mitihani yao wengi wao ni wale waliopelekwa english medium na wazazi wao. Ni wazi kabisa tutegemee maangamizi makubwa katika sekta ya elimu kama sera ya elimu itabaki kama ilivyo sasa.
 
We ushaambiwa kuna mkuu wa mkoa, mind you mkuu wa mkoa, Arusha huko, anakwepa kwenda kwenye mikutano kwa sababu hajui kiingereza.

Janga la kitaifa.
yaleyale ya you took my book, tookn't you?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…