Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Jaws Corner
Uchaguzi wa Zanzibar 1995
Propaganda kuhusu Maalim na siasa za Zanzibar zimezoeleka nyakati kama hizi.
Yaandikwayo hupati kusikia lolote la maana kutoka kwao.
Haya wasemayo yanavutia watu kutaka kusikiliza kwa kuwa Maalim Seif katajwa.
Tufanye "deduction" kama "experiment" ndogo tu.
Maneno haya haya ndani ya video clips "substitute" jina la Maalim na mwanasiasa mwengine uangalie huo ujumbe utawavutia wasomaji wangapi.
Hakuna.
Hiki ndicho kipimo cha ukubwa wa Maalim katika siasa za Zanzibar.
Maalim kakabiliana katika uchaguzi na marais wote waliotawala Zanzibar baada ya vyama vingi kuruhusiwa mwaka wa 1992.
Hili si jambo dogo - Salmin Amour, Amani Karume na Dr. Shein.
Matokeo ya chaguzi zote hizo tano zinafahamika.
Kalenda ya CUF Uchaguzi wa 1995
Ikionyesha tarehe ya kupiga kura na Maalim kuingia Ikulu Zanzibar
Hii ni historia ya pekee kabisa.
Hofu iliyokuwapo hivi sasa na hii ni wazi.
Itakuwaje endapo Maalim atagombea 2020 na atashinda.
Tunaweza kuangalia "trend," kisha tukaweka juu yake "Law of Probability."
Jibu ni jepesi mno.
Sayansi haisemi uongo.
Tushajua nini matokeo ya Uchaguzi wa 2020 Zanzibar.
Shinikizo la siasa Zanzibar haipo kwa Maalim wala kwa Wazanzibari wapiga kura.
Wazanzibari wanajua kutumbukiza kura ndani ya sanduku.
Wazanzibari siku zote wameonyesha dhahiri nini wanataka.
Propaganda hizi mitandaoni zinaonyesha hofu iliyoko visiwani.
Lakini zaidi zinawasaidia wenye kutumia akili zao na elimu ya sayansi kuelewa hali halisi iliyoko na inavyoikabali CCM yote Bara na Visiwani.
Ikifikia hapa kunakuja na maswali.
Zanzibar itaendelea hivi hadi lini?
Njia nyepesi ya kummaliza Maalim Seif na ndoto ya Wazanzibari waliyonayo kwa nchi yao ni CCM kumshinda Maalim kwenye sanduku la kura bila ajua na kufuta uchaguzi.
Lakini hii kuwa Maalim hawezekani kushindika katika kura, matatizo na hizi propaganda hazitakwisha kamwe.
Maalim ataendelea kuwashughulisha. CCM wamepatwa na maradhi ya "wishful thinking."
Wangependa kumuona Maalim anaangukiwa na mbingu.
"Legacy," atakayoacha Maalim hakuna kiongozi ataifikia hata siku moja katika miaka hii ya karibuni.
Wapi duniani kumekuwa na "immigration" ya wanachama wote na kiongozi wao kwenda chama kingine kwa siku moja tu?
Hii ni "Exodus." Hii ni "phenomenon," ambayo inaeleza yale ambayo CCM wanajitahidi kujifanya kuwa hayapo.
Lakini ukweli ndiyo huu.
Yapo.
Salama ya CCM Zanzibar iko katika kupitisha sheria itakayomzuia Maalim kutogombea.
Lakini hili nalo lina hatari nyingi sana.
Hatari yake ni kuwa CCM Zanzibar itakuwa imejiongezea nyoya jingine kichwani.
Nyoya la hofu ya kumuogopa Maalim na Wazanzibari raia wapiga kura.
Manyoya haya yatawaelemea sana kichwani - kushindwa kushinda kwenye kura, kushindwa kwa GNU, kufuta uchaguzi, kumzuia Maalim kugombea...
Sasa tufike kuwa Zanzibar chama kinabakia CCM peke yake kwa ajili ya hofu ya kuwa CCM katika ushindani haijiwezi.
Inashindwa kila uchaguzi visiwani.
Hapo sasa tunafungua mlango wa vurugu.