Zanzibar 2020 Maalim Seif aahidi Muungano Serikali 3

Zanzibar 2020 Maalim Seif aahidi Muungano Serikali 3

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mgombea urais wa Zanzibar kutia chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, ameendelea na kampeni zake katika kisiwa cha Pemba kwa ajili ya kuomba kura ili kupata nafasi ya kuongoza Zanzibar.

Akiwa Kiwani, mkoa wa Kusini Pemba, Maalim Seif aliwataka wananchi kumchagua ili kumpa nafasi ya kuleta mabadiliko ambayo yatahusisha muundo wa Muungano wa serikali tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Tanganyika na ya Zanzibar.

Alisema akichaguliwa anakusudia kufanya mazungumzo na Serikali ya Muungano kuhusu muundo wa Jeshi la Polisi ambalo ni taasisi ya Muungano ili yafanyike mabadiliko makubwa ikiwamo ajira kwa vijana.

‘’Nikichaguliwa kuwa Rais nakusudia kufanya mazungumzo na wenzetu wa Jamhuri ya Muungano kuhusu muundo wa Jeshi la Polisi na kuona linakuwa na sura ya pande zote mbili tofauti na sasa,’’ alisema.

Awali, Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Nassor Mazrui, aliwataka wananchi waikiwemo watumishi wa serikali kujitokeza kwa wingi kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 na kumchagua mgombea wanayemtaka bila ya kuwa na hofu.

‘’Acheni kujenga hofu kwa watumishi wa serikali, msiogope tumieni maamuzi yenu ya kuchagua kiongozi mnayemtaka wala msiogope,’’ alisema.

Naye aliyekuwa mgombea uwakilishi Jimbo la Ole kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Hamad Masoud, ambaye alienguliwa kugombea nafasi hiyo baada ya kuwekewa pingamizi, aliwataka wapigakura wa jimbo la Kiwani kuchagua mbunge na mwakilishi wa jimbo hilo kupitia chama hicho kwa ajili ya kuleta maendeleo.

‘’Nawaomba wananchi wa jimbo la Kiwani chagueni mwakilishi na mbunge kutoka chama cha ACT-Wazalendo kwa ajili ya kuleta maendeleo na mabadiliko makubwa ya kisiasa,’’ alisema
 
Sijui huyu mzee anatatizo gani anapambana Sana kuvunja muungano.
 
Sijui huyu mzee anatatizo gani anapambana Sana kuvunja muungano.
Anawakilisha mawazo ya wazanzibari walio wengi, you can count me on this one....well I am even worse I guess -> Sitaki muungano kabisa na Tanganyika. Tushirikiane kwa kupitia jumuiya ya afrika mashariki tuu.

P:S
Kukupa hint ya suprise tena mier personally nina family ties na watanganyika wakwe zangu wanatoke uko uko. Usije dhani labda nawachukia watanganyika haina maana hio kabisa.
 
Sijui huyu mzee anatatizo gani anapambana Sana kuvunja muungano.
Hivi wewe unamuelewa mleta Uzi?
''Akiwa Kiwani, mkoa wa Kusini Pemba, Maalim Seif aliwataka wananchi kumchagua ili kumpa nafasi ya kuleta mabadiliko ambayo yatahusisha muundo wa Muungano wa serikali tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Tanganyika na ya Zanzibar. ''

Jamii forum sikuhizi ime jaa vilaza
 
Back
Top Bottom