Naibu Waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni amemwagiza IGP Sirro kuwavua vyeo RPC wa Kusini pemba Hassan Nasir Ally na RPC wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohamed kwa kosa la kumwacha Jabali Maalim Seif kuhutubia wananchi wa Pemba , huku siasa za majukwaani zikiwa zimekatazwa
---
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Hamad Masauni amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kuwaondoa makamanda wawili wa polisi kisiwani Pemba kwa kushindwa kuzuia mikutano ya Mshauri wa chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad.
Masauni ametoa agizo hilo leo Alhamisi Desemba 12, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Unguja.
Amesema kwa muda mrefu kisiwa cha Pemba kimekuwa na matukio yasioridhisha jambo linaloashiria kuwa wameshindwa kazi.
Makamanda hao ni Hassan Nassir Ally wa Mkoa wa Kusini Pemba na Sheikhan Mohamed Sheikhan wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Akitoa mfano wa matukio hayo, Masauni amesema Maalim Seif anafanya mikutano kila kona huku ikijulikana kuwa imezuiwa.
Amesema sababu nyingine ni kutojengwa nyumba za polisi kisiwani humo licha ya Serikali kutoa maagizo.

Yule Dk Kigeugeu alipokuwa anafanya mikutano na masweta yake ya migomba hakuwa anafanya siasa? Hawa wanaishi kwa vitisho na mwisho wa kila mmoja umewadia.

Ndio maana tunasema ccm kwa sasa inategemea nguvu ya dola tu kufanya siasa. Na hii ndio inayopelekea jeshi la polisi kuvunja sheria kwa kuwakandamiza wapinzani ili kulinda vyeo.
Huo ni udhibitisho kuwa nguvu pekee ya ccm ni matumizi ya vyombo vya dola. Hizo hofu anazopandikiza huyo waziri, ndio huwafanya viongozi wengine wa jeshi la polisi kutii lolote wanaloogizwa dhidi ya haki za wapinzani, na wengine huenda mbali mpaka kufanya mauaji au kuleta vilema ili kulinda vyeo. Hivyo vyombo vya dola ndio pekee vinavyoendelea kulinda uwepo wa ccm hapa nchini.
Huku Kabudi anazunguka anaiambia Dunia kuwa mikutano ya kisiasa Tanzania haijazuiliwa muda huo huo kuna mtu anaagiza polisi wafukuzwe kushindwa kuzuia mikutano ya kisiasa,mnafikiri hawajui kinachoendelea Tanzania ,Sithole State