Uchaguzi 2020 Maalim Seif Sharif: Helicopter zitakuwa zinatembea zitafanya kazi ya kuwalinda wavuvi wetu

Uchaguzi 2020 Maalim Seif Sharif: Helicopter zitakuwa zinatembea zitafanya kazi ya kuwalinda wavuvi wetu

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
MGOMBEA Urais Zanzibar kupitia tiketi ya ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad amekutana na wavuvi na wakulima wa Mwani na Kijiji cha Tumbe, mkoa wa Kaskazini Pemba na kuwahidi kuwapa vifaa vya kisasa na ulinzi wa kuwalinda nyakati za uvuvi.

Maalim Seif alitoa ahadi hiyo wakati akisikiliza changamoto zinazowakabili na kushauriana njia bora za kutatua changamoto hizo.

Baadhi ya wavuvi na wakulima walilalamikia bei ya Mwani ambayo ni shilingi 600 kwa kilo na ukosefu wa vyombo vya kisasa vya uvuvi.

“Serikali ya ACT Wazalendo chini ya Maalim Seif Sharif Hamad itashugulikia suala hilo, mtapata hivyo vyombo bila ubaguzi, vyombo hivyo vitakua na spidi kubwa na kama alivyosema Mazrui na Helicopter juu zitakua zinatembea zitafanya kazi ya kuwalinda wavuvi wetu,” amesema Maalim Seif.

Awali akizungumza kwenye mkutano huo wa wavuvi na wakulima, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Nassor alisema “Tumejiandaa kuhakikisha kua vijana wetu tunawapa mafunzo, mitaji na zana za kuvulia. Hayo yamo katika ilani yetu, suala la muhimu hapa ni kumfikisha Maalim ikulu,” Mazrui Nassor.

HabariLeo
 
Gooo Maalim Gooo ... Taifa letu kwa muda sasa limekosa viongovi wa wananchi badala yake tumepata watawala wenye uchu wa Madaraka na kukalia Taifa kimabavu bila ridhaa za wananchi.
 
Awali akizungumza kwenye mkutano huo wa wavuvi na wakulima, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Nassor alisema “Tumejiandaa kuhakikisha kua vijana wetu tunawapa mafunzo, mitaji na zana za kuvulia. Hayo yamo katika ilani yetu, suala la muhimu hapa ni kumfikisha Maalim ikulu,” Mazrui Nassor
Yooooote haya tayari yanafanywa na CCM
 
Back
Top Bottom