Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MAALIM: "THE GREATEST OF ALL TIME" KUTOKA CUF HADI ZAMBARAU
Washehereshaji wa masumbwi Muhammad Ali alipokuwa ulingoni waliongeza kibwagizo katika kumtambulisha.
Baada ya kutaja jina lake waliongeza maneno haya, "The Greatest of all time," yaani hakuna wa kumfikia kwa nyakati zote hadi mwisho wa dunia.
Kibwagizo hiki walimpa katika miaka yake ya mwanzo baada ya Ali kupigana na kila bingwa kutoka kila pembe ya dunia na kuwashinda wote.
Walikuwapo Marekani mabingwa wa uzito wa juu kabla yake lakini hakuna aliyevishwa taji hili.
Tuingie kwa Maalim Seif.
Haikutegemewa kuwa CUF itapata nguvu ilikuja kupata nguvu illiyokuja kupata Bara.
CUF bara kilikuwa chama masikini lakini walikuwa na wanachama waliokuwa na ari kubwa isiyosemeka.
Hapakuwa na chama ambacho wanachama walikuwa wakichangishana fedha kukodi magari kuhudhuria mikutano yao.
Kila mtaa kulikuwa na tawi la CUF na "vijiwe,"" na wenyewe wakitoa matawi na vijiwe vyao majina ya kuvutia na kugonga nyoyo.
Kulikuwa na vijiwe na matawi yaliyoitwa "No Retreat No Surrender," Bosnia, Cosovo nk.
Wanachama wa CUF wengi wao walikuwa watu wa aina moja kutoka jamii moja na wakifanana kwa mengi.
Mikutano ya CUF ikivutia utadhani "carneval" ya Brazil.
Juu ya matatizo waliyokuwa wanakutananayo wanachama na viongozi wa CUF hawakufa moyo.
Kila aina ya propaganda ilivurumishwa dhidi yao na vyombo vya habari kwa kuitwa CUF ni chama cha Waislam, hii badala ya kuidhoofisha CUF ilizidi kutia nguvu.
Maalim Zanzibar akawa inashinda kila uchaguzi kila mgombea urais wa CCM akawa anaangushwa na CCM.
CCM iliingia katika uchaguzi wa mwaks wa 2000 wakiwa na kumbukumbu ya kipigo walichopata mwaka wa 1995.
Hii ilikuwa sawa na pigano la pili la Muhammad Ali na Sonny Liston baada ya kuvuliwa mkanda na Muhammad Ali wakati huo Cassius Clay.
Liston alipanda ulingoni akiwa na kumbukumbu ya kipigo alichopata pambano lililopita.
Nilikuwa nimetabiri huko nyuma kuwa CCM Zanzibar haitaweza kushinda uchaguzi visiwani.
Katika miaka mitano ile ya utawala wa Salmin Amour nilizidi kuamini kuwa na uchaguzi wa 2000 CCM Zanzibar itashindwa tena.
Kwa nini niliamini hivi.
CCM Zanzibar na yeye Salmin Amour walikataa kuamini kama alishindwa uchaguzi akawa yeye na chama chake wanajichukulia kama walishinda uchaguzi kwahiyo hapakuwa na matayarisho yoyote ya kuvutia wapigaji kura waliomkataa waje wampigie kura mrithi wake wakipe chama ushindi.
Sikuwa naamini kama hili CCM walikuwa hawalijui kuwa wataingia ulingoni na bondia ambae tabu kumshinda.
Ikiwa nilikuwa naamini kuwa CCM wameshaonja kushindwa lakini hawana matayarisho ya kupata ushindi nini wanategemea kitawapa ushindi?
CCM Zanzibar ilikuwa sasa imeshatambua nguvu ya sanduku la kura.
Lakini walikuwa pia wanafahamu kuwa ipo nguvu nyingine yenye uwezo mkubwa kushinda nguvu ya sanduku la kura lau kama nguvu hii imebaba hatari kubwa.
Sikupata tabu kutambua na pengine kwa kukosa kutambua nafasi ya demokrasia duniani CCM Zanzibar pakasikika maneno ya kusema tena ndani ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania kuwa hata wakishindwa hawatatoa serikali.
Kitu cha kusikitisha kauli hii ilipokelewa kwa vifijo na wabunge.
Kwangu mimi huu ulikuwa uthibitisho kuwa CCM Zanzibar tayari imeshatambua nguvu ya Maalim na kauli zao sasa zinathibitisha.
Ukweli umewadhihirikia kuwa hawana uwezo wa.kumshinda Maalim.
Na hivyo ndivyo ilivyotokea katika uchaguzi wa mwaka wa 2000.
Yaliyotokea sote tunayajua.
Mapinduzi yakawa sasa ni ghali sana kwa Wazanzibari.
Hakuna mtawala anaejisikia vyema kukalia kiti kinachovuja damu za raia wake.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ilileta matumaini mapya Zanzibar.
Matumaini haya yote yalipeperushwa na uchaguzi wa 2015.
Maalim akashinda tena na uchaguzi ukafutwa.
Marehemu Bi. Asha Bakari alipata kusema, "Hatutoi, hatutoi, hatutoi."
Na hivi ndivyo ilivyokuwa.
Ikafuatia kwa CUF kuporomoka na Maalim na wafuasi wake wakawa wanahangaika wakisubiri uamuzi wa mahakama.
Uamuzi wa mahakama uliwaendea vibaya CUF Maalim akajikuta hana chama.
CCM Zanzibar ilipumua kwa furaha.
Maalim akifanya kitu hakijapata kutokea duniani.
Nimehangaika sana kuwauliza marafiki zangu kwenye vyuo vingi duniani kama kuna mahali kitu kama hiki kimetokea.
Sijapata jibu.
Baina ya Dhuhr na Maghrib Maalim alitoka CUF na wanachama takriban wote na ofisi zote zilizokuwa za CUF zikawa zimepakwa rangi ya zambarau ya ACT Wazalendo.
Huu ukawa ndiyo mwisho wa CUF Zanzibar na Bara.
Maalim akaingia uchaguzi wa 2020 akiwa na chama kipya.
Hakuna kilichopungua wala kubadilika katika nguvu na ushawishi wa Maalim kwa Wazanzibari.
Uchaguzi wa 2020 umefungua ukurasa mpya si Visiwani bali hata Bara.
Yaliyotokea hayajapata kutokea.
And Maalim The Greatest of all time is still standing.