#COVID19 Maambukizi mapya ya UVIKO-19 yatajwa kuongezeka Nchini

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Serikali imetangaza mwenendo wa ugonjwa wa Uviko-19 nchini kwa kipindi cha Oktoba 29 hadi Desemba 2 huku takwimu zikionyesha wanaougua wakiongezeka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 5, 2022 na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu, visa vipya vya maambukizi ya Uviko-19 vilivyobainika ni 442.

Profesa Nagu amesema katika taarifa yake kwamba idadi hiyo ni kubwa ukilinganisha na takwimu za mwezi uliopita ambapo kulikuwa na visa vipya 272, sawa na ongezeko la asilimia 62.5 na kwa kipindi hiki hakuna mgonjwa aliyelazwa wala kifo.

“Serikali imeendelea kutoa huduma za chanjo ya Uviko-19 nchini ili kuwawezesha wananchi kupata kinga kamili na hivyo kuzuia kupata ugonjwa mkali na hata kifo pale mtu anapopata maambukizi ya virusi vinavyosababisha Uviko-19,” amesema Profesa Nagu katika taarifa yake.

Amesema hadi kufikia Desemba 2 mwaka huu, jumla ya watu 29,123,387 kati ya walengwa 30,740,928 ambao ni sawa na asilimia 94.7 wamepata dozi kamili ya chanjo ya Uviko-19.

“Wizara inawahimiza watu wote wenye dalili za magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa kama vile homa, mafua, kikohozi, mwili kuchoka, maumivu ya viungo, kuumwa kichwa, vidonda vya koo, kupumua kwa shida kwenda vituo vya kutolea huduma za afya mapema ili kuweza kupimwa na kupatiwa matibabu stahiki,” inaeleza taarifa hiyo.

Amesema wizara inaendelea kutoa tahadhari kwa wananchi wote kuchukua hatua za kujikinga na Uviko-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na kupata dozi kamili za chanjo ya Uviko-19, kuvaa barakoa pindi unapokuwa na dalili za mafua au kikohozi na uwapo kwenye mikusanyiko.

“Pia kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka mara kwa mara, kuendelea kuchukua hatua za kujenga mwili imara kwa kufanya mazoezi na kula vyakula bora, kujenga tabia ya kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya endapo utajihisi u mgonjwa, kutoa taarifa za kuwepo watu wenye dalili za magonjwa katika jamii kupitia namba ya simu ya bure y 199,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
30,740,928 ambao ni sawa na asilimia 94.7 wamepata dozi kamili ya chanjo ya Uviko-19.

Kwa data hizi mlisema watanzania wapo 61 milioni? Au

Kwa hiyo 1/2 ya watanzsnia wamepata chanjo?
 
HUO NI UONGO WA KIWANGO CHA SGR!!

WANATAFUTA SABABU YA KUPATA MIKOPO[emoji849][emoji849]
 
Serikali imetangaza mwenendo wa ugonjwa wa Uviko-19 nchini kwa kipindi cha Oktoba 29 hadi Desemba 2 huku takwimu zikionyesha wanaougua wakiongezeka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 5, 2022 na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu, visa vipya vya maambukizi ya Uviko-19 vilivyobainika ni 442.

Profesa Nagu amesema katika taarifa yake kwamba idadi hiyo ni kubwa ukilinganisha na takwimu za mwezi uliopita ambapo kulikuwa na visa vipya 272, sawa na ongezeko la asilimia 62.5 na kwa kipindi hiki hakuna mgonjwa aliyelazwa wala kifo.

“Serikali imeendelea kutoa huduma za chanjo ya Uviko-19 nchini ili kuwawezesha wananchi kupata kinga kamili na hivyo kuzuia kupata ugonjwa mkali na hata kifo pale mtu anapopata maambukizi ya virusi vinavyosababisha Uviko-19,” amesema Profesa Nagu katika taarifa yake.

Amesema hadi kufikia Desemba 2 mwaka huu, jumla ya watu 29,123,387 kati ya walengwa 30,740,928 ambao ni sawa na asilimia 94.7 wamepata dozi kamili ya chanjo ya Uviko-19.

“Wizara inawahimiza watu wote wenye dalili za magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa kama vile homa, mafua, kikohozi, mwili kuchoka, maumivu ya viungo, kuumwa kichwa, vidonda vya koo, kupumua kwa shida kwenda vituo vya kutolea huduma za afya mapema ili kuweza kupimwa na kupatiwa matibabu stahiki,” inaeleza taarifa hiyo.

Amesema wizara inaendelea kutoa tahadhari kwa wananchi wote kuchukua hatua za kujikinga na Uviko-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na kupata dozi kamili za chanjo ya Uviko-19, kuvaa barakoa pindi unapokuwa na dalili za mafua au kikohozi na uwapo kwenye mikusanyiko.

“Pia kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka mara kwa mara, kuendelea kuchukua hatua za kujenga mwili imara kwa kufanya mazoezi na kula vyakula bora, kujenga tabia ya kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya endapo utajihisi u mgonjwa, kutoa taarifa za kuwepo watu wenye dalili za magonjwa katika jamii kupitia namba ya simu ya bure y 199,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
covid 19 bado ipo na mahospitalini wapo wagonjwa, ila hawasemi na si nyingi na kali kama zamani... ipo, ipo ipo! Vaeni barakoa!
 
Hii issue Ni kweli wadau hasa huku Zanzibar watu wanaumwa Sana Ila uzuri Ni kwamba Wana recover fresh tu Sio kama wimbi lililopita ambapo wengi walipoteza Maisha.
 
baada ya kuona kesi ya mabehewa kuwa juu wanaleta la uviko-19 wakati wenyewe wanasema hakuna kipindi cha jiwe.
ccm hii na familia yangu atakayekuwa ccm undugu basi
 
Serikali imetangaza mwenendo wa ugonjwa wa Uviko-19 nchini kwa kipindi cha Oktoba 29 hadi Desemba 2 huku takwimu zikionyesha wanaougua wakiongezeka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 5, 2022 na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu, visa vipya vya maambukizi ya Uviko-19 vilivyobainika ni 442.

Profesa Nagu amesema katika taarifa yake kwamba idadi hiyo ni kubwa ukilinganisha na takwimu za mwezi uliopita ambapo kulikuwa na visa vipya 272, sawa na ongezeko la asilimia 62.5 na kwa kipindi hiki hakuna mgonjwa aliyelazwa wala kifo.

“Serikali imeendelea kutoa huduma za chanjo ya Uviko-19 nchini ili kuwawezesha wananchi kupata kinga kamili na hivyo kuzuia kupata ugonjwa mkali na hata kifo pale mtu anapopata maambukizi ya virusi vinavyosababisha Uviko-19,” amesema Profesa Nagu katika taarifa yake.

Amesema hadi kufikia Desemba 2 mwaka huu, jumla ya watu 29,123,387 kati ya walengwa 30,740,928 ambao ni sawa na asilimia 94.7 wamepata dozi kamili ya chanjo ya Uviko-19.

“Wizara inawahimiza watu wote wenye dalili za magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa kama vile homa, mafua, kikohozi, mwili kuchoka, maumivu ya viungo, kuumwa kichwa, vidonda vya koo, kupumua kwa shida kwenda vituo vya kutolea huduma za afya mapema ili kuweza kupimwa na kupatiwa matibabu stahiki,” inaeleza taarifa hiyo.

Amesema wizara inaendelea kutoa tahadhari kwa wananchi wote kuchukua hatua za kujikinga na Uviko-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na kupata dozi kamili za chanjo ya Uviko-19, kuvaa barakoa pindi unapokuwa na dalili za mafua au kikohozi na uwapo kwenye mikusanyiko.

“Pia kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka mara kwa mara, kuendelea kuchukua hatua za kujenga mwili imara kwa kufanya mazoezi na kula vyakula bora, kujenga tabia ya kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya endapo utajihisi u mgonjwa, kutoa taarifa za kuwepo watu wenye dalili za magonjwa katika jamii kupitia namba ya simu ya bure y 199,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
Matamko ya serikali hii ya sasa sio ya kuyaamini sana.
 
Kuna mkopo kutoka kwa mabeberu unatafutwa hapa
 
Back
Top Bottom