Maambukizi ya UKIMWI: Mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya inaongoza

THE GREAT CAMP

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2012
Posts
765
Reaction score
194
Viwangovyamaambukizi ni vikubwa zaidi katika mikoa ya Njombe (14.8%), Iringa na Mbeya (9%) na ni vyachini zaidi Zanzibar na Manyara.

Nchi nzima, 5.1% ya wanawake na wanaume wenye miaka 15-49 wana maambukizi ya VVU. Wanawake wana kiwango kikubwa cha maambukizi kuliko wanaume mijini na vijijini. 7.2% ya wakazi wa mijini wana maambukizi ya VVU ukilinganisha na 4.3% ya wakazi wa vijijini.

FUNGUA HIYO ATTACHMENT HAPO CHINI UONE TAKWIMU ZA MIKOA YOTE.


SOURCE: Utafiti wa Viashiria vya VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania 2011-12
 

Attachments

Ahsante kwa taarifa hiyo muhimu,hata hivyo jitahidi kuweka nafasi kati ya neno moja na lingine maana unaonekana ni darasa la pili B. NB; Kwa Njombe imeniuma sana maana ndugu zangu sasa ndio majanga!

ELIMU YA UKIMWI IZINGATIWE NYEVAAA! Ulusungu lunya vanu kuutalo kuli mbulago!
 
.... Tulizana!
Takwimu za jiji la Dar es Salaam je?
 
Njombe na makete noma,yaani ngoma huku ndio maleria yetu.wakati dar mnapiga foleni hospitali kisa malaria,huku watu wanapiga foleni hospitali kisa ngoma.for tge first time nilipofika njombe i was shoked,ila nilikujakubloo mwenyewe nilipoenda hospitali ya ikonda makete.acheni jamani,kunahitajika nguvu ya ziada huku.ugimbi,na ulanzi huku,mambo ya kuangushana kwenye vitindi na baridi la huku vinachangia sana.
 

KILIVITE nakuheshimu sana, na naheshimu mawazo yako. Nimeweka maandishi kama yalivyo kwenye Report, nime-edit zaidi ya mara 3, lakini ukipost maandishi yanarudi vilevile kimbanano.Kuhusu Elimu yangu inawezekana ikawa nikweli darasa la Pili B. Chamsingi anaglia huo ujumbe aliokuwekea huyo std IIB mantiki yake. Otherwise TUKO PAMOJA . Tushirikiane kupambana na UKIMWI.
 
Asante the Great. Je unaweza kuipata ripoti yote ukairusha hapa?

Sawa ngoja niangalie modality ya kuwawekea summary report.Ingawa niliweka hiyo attachment ukiifungua ina ramani ya TZ ikionyesha takwimu za UKIMWI kwa kila mkoa.
 

ahsante ndugu,nimekukubali!IT BEGINS WITH US!
 
Sawa ngoja niangalie modality ya kuwawekea summary report.Ingawa niliweka hiyo attachment ukiifungua ina ramani ya TZ ikionyesha takwimu za UKIMWI kwa kila mkoa.

Asante sana. Nimeiona hiyo summary ya mikoa. Lakini ripoti nzima si unajua mkuu inaongeza hata utamu wa kusema kitu
 
Asante sana. Nimeiona hiyo summary ya mikoa. Lakini ripoti nzima si unajua mkuu inaongeza hata utamu wa kusema kitu
nime weka summary report kwenye original thread hapo juu.Angalia hiyo PDF doc. Mkuu report nzima ina page kama 300 hivi.
 
Hali ni mbaya.... Ila huwa sielewi inakuaje mwanza na tanga bado zina asilimia ndogo wakati ni mikasi kwa kwenda mbele
 
Mdau THE GREAT CAMP
Nimepitia hii attached document sijaona watafiti wakitupa sababu za ukubwa wa tatizo katiko hizo top three na 'unafuu' katika hiyo mikoa mingine. Tafadhali kama una madodoso zaidi naomba utusaidie ili kulifahamu tatizo kiundani.

N.B
Mikoa ya Iringa na Njombe ina idadi kubwa sana ya taasisi za kiraia(local and international) zinazofanya public awareness ya HIV/AIDS. Je huku ni kufeli kwa mbinu/mikakati/malengo/dira za miradi ya hizi taasisi!!????
 
Last edited by a moderator:
Sawa nitaweka summary zingine zinazo onyesha sababu mbalimbali za hali hizo
 
Kwa nyongeza,takwimu hizo zinapatikana kwenye website ya nbs (nbs.go.tz),takwimu alizozizungumzia mleta mada zipo.
Aidha takwimu za idadi ya watu katika mikoa,wilaya hadi kata,pamoja na idadi ya watu by sex.
 
ili kuinusuru Njombe; kama hii program ya DONDOSHA MKONO WA SWETA kwa wakazi wa Njombe ikishindwa kuleta expected results itabidi ianzishwe nyingine itakayokuwa inajulikana kama FUNIKA KISIMA special kwa akina mama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…