Maambukizi yaongezeka nchini, Dar es Salaam yaripoti visa 130

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya kuanzia Mei 05 - Juni 03, maambukizi mapya 161 yamerekodiwa ikiwa ni ongezeko la 137% ikilinganishwa na kipindi cha Aprili 02 - Mei 04, 2022

Dar imeripoti visa 130, Arusha (10), Mwanza (5), Shinyanga (4), Mtwara (3), Dodoma (2), Mara (2), Morogoro, (1), Simiyu (1), Katavi (1), Kilimanjaro (1) na Mbeya (1)



 
Enhee, lete fungu siumeona.
 
Tunakoholeana sana na chafya kwenye mwendokasi, hivyo mafua na vifua (TB) kwa wakazi wa dar vitatuandama sana tusipo chukua tahadhari.

Ila hii ya uviko mmmh...inafikirisha sana.
 

Kazi imeanza rasmi. Kesho watafika 678 nchi nzima
 
Wanataka tutengwe na dunia? Ukizingatia hiki ni kipindi cha ibada ya hija?
Acheni ugalatia wenu aisee
 
Nchi ya Vice Versa..., Wakati kweli baridi inatupiga tulitupa mashuka...., sasa hivi jua linawaka ndio tunahimizana kuvaa makoti....

Ajabu ni kwamba hao wahimizaji at that time (wakati tunapigwa na baridi) walikuwa wanatembea vifua wazi kwamba joto limezidi
 
Jana wamepita mitaa ya mbezi walipita mitaani wanachanja nyumba hadi nyumba, watu wanawashangaa tu,
 
Msimu wa baridi huu na watu kupuuza kujifanya covid 19 haipo.
 
Hamjachoka tu na Mambo ya uviko huo tumeuweza
 
Hayo ni maagizo kutoka kwa mabeberu wameona igizo lao la corona limefunikwa na vita ya Urusi.....

Mungu amuepushie magufuli adhabu za kaburi Aamen!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…