Nduna Likapo
Member
- Apr 25, 2013
- 97
- 19
Wanajamvi siku 2 sasa zimepita toka Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba atoe tamko mbele ya waandishi wa habari na akisisitiza kauli yenye utata na giza nzito ya kwamba Tume yake itafanya maamuzi magumu kutokana na kuwepo na maoni mengi yanayotofautiana toka kwa wananchi.Kauli hii ni tata inayohitaji mjadala wa kina kwa usalama wa taifa letu.Binafsi baada ya kufanya tathimini nimeshindwa kumuelewa mzee Warioba kwa yafuatayo.(1) Ni maamuzi yapi magumu watakayoyafanya kwenye katiba ya watanzania?haya maamuzi magumu hayatakuwa na harufu ya kulibeba kundi flani katika jamii?je hayo maamuzi hatakuwa na mkono wa wanasiasa na watawala?Watanzania tumeshafanya maamuzi magumu na kwa kutoa maoni kwa yale tunayoyataka na tume itimize wajibu wake na sio kutuzungusha na kauli zenye utata.Namuheshimu sana Mzee warioba na tume yake,Lakini wao kama tume hawatakiwa kuja na kauli zenye giza kwa wananchi,kazi ya tume ni kukusanya na kuyaratibu maoni ya watanzania na sio kufanya maamuzi magumu tusiyoyajua watanzania ni yapi.Huu ni Mtazamo wangu,Sijui wewe unafikiria nini kuhusu maamuzi magumu ya Mzee Warioba na Tume yake.Mungu ibariki Tanzania.