Inaonekana rufaa zote zimekataliwa na hii TumeCCM hapo Mbeya mjini (Mahera anajua fika CCM haina chake Mbeya). Na imenishtua sana hapo Babati mjini eti rufaa nne za wagombea ubunge walioenguliwa kutoka vyama vinne tofauti zimekataliwa. Huu ni mpango mkakati wa TumeCCM kumpitisha msaliti Pauline Gekul bila kupingwa!. Vyama husika visinyamazie uovu huu! Hivi vyama husika (najua wagombea wa Chadema na ACT watakuwa miongoni mwa walioenguliwa) vinahitaji kuanika uovu huu wa TumeCCM ili waangalizi huru wa uchaguzi na dunia ijue hakuna tume huru ya kutenda 'haki' hapa Tanzania!