Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
kwa muda mrefu sana nimekuwa ninaamini kuwa bingwa ni yule anayeshinda wote katika vigezo vinavyotambulika, na ni lazima ubingwa wake uambatane na vigezo hivyo. Kwa mfano "Bingwa wa ndondi za uzito wa juu," "Bingwa wa mpira wa miguu barani afrika," BBingwa wa kucheza ngoma za kizaramo" na kadhalika. Ubingwa hupatikana kwa kushindanisha watu au makundi kadhaa katika kigezo kinachousika. mabingwa ndio wanaoitwa kwa lugha za wenzetu kuwa Champion, yaani aliyeshinda wote. Bingwa anaweza kuupoteza ubingwa wake kwa kushindwa na wengine, na vile vile kuupata tena kwa kuwashinda waliomnyanganya.
Mara nyingi nimekuwa nasoma wataalamu wanaoitwa madatari Bingwa ambao ni specialists, na hapo ndipo ninaposhindwa kuelewa matumizi ya hilo neno bingwa kuhusiana na wataalamu wa kusomea. Je nao huwa wanashindanishwa na kuwazidi wengine wote, na je wanaweza kuupoteza ubingwa huo kama walivyo machampioni wengine? Wakati wasomea hiyo specialty yao tutasema kuwa "wanashindania ubingwa" fulani? Je kwa kiswahili neno "specialize" litakuwaje?
Naomba msaada