Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,777
Wandugu, kuna misconception miongoni mwa Watanzania wengi niliokutana nao (na michango inayoletwa hapa) kuhusu lockdown (kuzuia watu wao kutoka majumbani kwao kwa kiwango fulani) ikiwa ni moja ya hatua za kupambana na COVID 19 pandemic. Nchi zote ambazo zimetangaza kuwa hadi sasa zimefanikiwa kuzuia maambukizi mapya ya coronavirus zikiwemo Taiwan na New Zealand zilitumia njia hii.
Kuna nchi ambazo ziliingia kwenye lockdown (hazijtangaza kuwa coronavirus free hadi sasa) zimeanza kulegeza zuio la watu kukaa majumbani mwao. Kuna nchi nyingine (ikiwemo Tanzania) ambazo hazikuingia kwenye lockdown.
Kinyume na imani ya Watanzania walio wengi (niliokutana nao au kusikia michango yao) lockdown haimaanishi kuwa watu wanazuwiwa kutoka majumbani mwao 100%. Haimaanishi pia kutofanya kazi au kuzuia magari ya mizigo. Watu walio kwenye lockdown wanaruhusiwa kutoka ili kufanya shughuli muhimu kwa mfano; kwenda bank, pharmacy, supermarket etc, etc.
Hitimisho: Tanzania sasa hivi ipo kwenye Lockdown ya kulazimishwa na majirani zetu (sasa hivi ni kama 70%). Malawi nao wakifunga mpaka wao na sisi tutakuwa tupo kwenye 98% lockdown - Msumbiji hatuna biashara kubwa sana nao inayohusisha usafirishaji wa mizigo. Tungechukua hatua hiyo wenyewe tungekuwa kwenye hali bora zaidi kuliko tutakayokuwa nayo tuendako.
Let's wait and see.