Maana halisi ya Rastafari

umenikumbusha hii vybz ngoja ni pakue kwanza
 

Amen [emoji1545]
 
Ni kiongozi wetu wa kiimani

Haile Sellasie - Maana yake Holy Trinity, yaani Utatu Mtakatifu!
Hii Imani ya Marasta ni Mchanganyiko wa Ujudaism na imani ya madhehebu ya Kicoptic Ambayo Imani hii imekuwepo Ethiopia kabla ya Wazungu hawajafikiwa na Ukristo pamoja na Uislam kuanza kua Imani kuu mashariki ya Kati na kwingineko.

Ingawaje imetohoa doctrine zake toka katika Imani hizi,Rastafarianism imekuwepo kwa Muda mfupi tu si zaidi ya miaka 75! lakini imepata umaarufu mkubwa ulimwenguni.
Kimsingi Hawa Jamaa Wanaamini katika Amani na Upendo na Kuhusudu sana Mmea Mmoja wa Kimiujiza - Cannabis Sativa,Hashish,Weed,Ganja.

Kwa Mtindo wa Maisha ni Vegetarians,Hawagusi Nyama wala Kuua kiumbe chochote,hivyo kwa mantiki hii wanafanana na Majainist wa India.
Hivyo Hii siyo Imani mpya! Ni aina flani ya Mkusanyiko wa Theolojia ya Imani Mbalimbali toka dini zingine,hasa Abrahamic religions.
Wanaamini matatizo mengi yanaletwa na Utawala Usio wa Haki Duniani hasa Western Nations (Babylon System).

Rastaman never die,
When Die cannot decay,
When decay cannot smell,
When Smell,smells like a perfume.

Kuhusu Kuwa Imani Timilifu Sijui!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…