SoC02 Maana halisi ya Taifa la kesho na kuliandaa

SoC02 Maana halisi ya Taifa la kesho na kuliandaa

Stories of Change - 2022 Competition

Bashir Habib

New Member
Joined
Sep 4, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Moja katika rasilimali ya Taifa ambayo ni muhimu sana kuifahamu ni vijana, hawa ndio nguvu kazi ya Taifa Kwa muda wa sasa na hata wa badae.

Lakini pia watoto ni nguvu kazi ya Taifa Kwa muda wa baadae.
Hvyo watoto na vijana ni jamii ya watu watakaoishi baadae kwa uendeshaji wa maisha Yao Kwa kutegemea fikra zao wenyewe.

Ni jukumu la wazazi na wasimamizi wote wa jamii hizi kuhakikisha wanawatengenezea mustakabali mwema wa majukumu yao ya kuendesha nchi kwa muda wa badae. Na jamii hii ndio imeitwa "Taifa la kesho".

Maendleo na matokeo chanya katika nyanja zote tunayoyashuhudia na kunufaika na nayo hivi leo katika maisha yetu ya sasa, ni dhahiri kuwa yametokana na maandalizi na mipango bora iliyopangwa katika wakati uliopita kabla ya leo. Na ndio maana leo tunanufaika na wafanyakazi wa umma wenye Tija katika jamii ikiwa ni pamoja na viongozi bora wenye ukomavu katika siasa,watumishi wa wizara ya afya wenye weledi mzuri, lakini pia tunashuhudia kupanda Kwa uchumi na miundo mbinu iliyo mizuri ya kudhibiti kudumaa kwa hali ya kiuchumi n.k. Ambapo kinyume chake katika nyanja zote hizo kuna baadhi ya mapungufu ambayo tunayashuhudia wakati mwingine hujitokeza kama vile; Uongozi na tawala bila ya weledi, huduma hafifu katka nyanja za afya na elimu katika jamii, kuzorota kwa hali ya uchumi katika baadh ya jamii.

Hivyo Kuna ulazima na umakini katika kuliandaa Taifa la kesho katika misingi iliyo bora, ili kutengneza mustakabali mzuri wa maisha ya baadae.

Maana halisi ya Taifa la kesho ni jamii tunayoishi nayo sasa itakayobeba majukumu ya kuliendesha Taifa kwa baadae Kwa kutegemea misingi ya maandalizi katika muda wa Maisha Yao ya sasa, kielimu,kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.

Bila shaka hii jamii inayoishi leo hapana budi kuhakikisha inafanyiwa maandalizi mazuri, yaani ipewe haki zote za msingi zitakazoiwezesha kuwa Taifa bora la kesho. Jamii hii inayotarajiwa kuwa Taifa la kesho iandaliwe katika nyanja mbali mbali za kijamii kama vile;

ELIMU:
Jamii inayotarajiwa kuwa Taifa la kesho ni lazima ipewe elimu ya kutosha na iliyo bora kwa wakati wa sasa kabla ya kuingia katika majukumu ya kitaifa Kwa kuzingatia mazingira bora ya kujifunzia na mahitaji yote ya msingi kama chakula, malazi, vifaa vya kujifunzia n.k.

UCHUMI:
Jamii inayoandaliwa ipewe mafundisho na majaribio ya vitendo katika kuhifadhi vyanzo vya uchumi kama vile; uvuvi,viwanda,kilimo n.k

SIASA:
Jamii inayoandaliwa kuwa Taifa la kesho ijengewe misingi ya kujiamini katika kusimamia hoja, uzalendo,kujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya maslahi ya nchi na kusimamia haki baina yao na hata kwa jamii nyingine.

UTAMADUNI
Jamii iandaliwe kifikra na kupewa fikra sahihi inayoweza kuleta tija katika taifa, na iondolewe katika fikra ambazo zinaweza kupelekea kuzorota kwa maendleo ya Nchi kama vile; kutokujishughulisha na shughuli za kujenga Taifa kwa mazoea ya kukaa vijiweni,kukeketa watoto wa kike ambapo inaweza kuleta madhara pia hata kusababisha vifo, kutokuwapeleka wagonjwa katika vituo vya afya na badala yake kubaki nao nyumbani Kwa madai ya kuwa wao ndio wenye tiba halisi, Jambo ambalo si sahihi.

Ni muhimu sana kuliandaa Taifa la kesho katika misingi ya kizalendo na iliyo bora. Kwa kufanya hivyo tutapunguza ama kuondosha kabisa adha na matatizo yanayotukumba Leo katika nyanja za kielimu, uchumi,siasa na utamaduni.

Na Bashir
 
Upvote 0
Back
Top Bottom