Zakaria Maseke
Member
- Apr 26, 2022
- 83
- 128
Unapoandaa affidavit au kiapo unatakiwa kuapa juu ya mambo ambayo yako kwenye ufahamu wako binafsi tu. Soma Order XIX rule 3(1) Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (CPC) inasema, "#Affidavits_shall_be_confined_to_such_facts_as_the_deponent_is_able_of_his_own_knowledge_to_prove..." Hata hivyo, unaruhusiwa kuapa taarifa ambazo haziko kwenye ufahamu wako ila hakikisha unataja chanzo chake.
Kwenye sehemu ya uthibitisho wa kiapo chako au hata ukiandaa nyaraka yoyote ambayo ina kifungu cha kuapa/uthibitisho/verification clause mfano plaint, wakati unathibitisha unatakiwa utaje bayana, aya zipi ni taarifa unazozijua wewe binafsi na kama kuna taarifa za kuambiwa, ainisha aya zipi ni habari za kuambiwa na ni nani aliyekuambia na utamke kabisa kuwa hayo uliyoambiwa unayaamini kuwa ni kweli.
Ukithibitisha tu juu juu eti "yote niliyosema hapo juu ni kweli tupu kadiri ya ufahamu wangu binafsi" ukaishia hapo wakati kuna aya umechanganya na taarifa za kuambiwa, kiapo chako kinakua batili. "The law does not allow a blanket or rather a general verification" Na ukithibitisha kuwa yote niliyosema ni kweli tupu kadiri ya ufahamu wangu binafsi na imani (belief) bila kutaja aya zipi zinatokana na imani (belief) na chanzo chake, kiapo chako kitakua batili.
Hii ni kwa mujibu wa kesi nyingi sana ikiwemo hii ya Mahakama ya Rufani, kati ya ANATOL PETER RWEBANGIRA na PRINCIPAL SECRETARY, MINISTRY OF DEFENCE AND NATIONAL SERVICE, CIVIL APPLICATION NO. 548/04 OF 2018. (Hakuna nyaraka ngumu kuandaa kama kiapo. Kama intern humwamini usimpe hii kazi. Haya ni machache tu kati ya masharti ya affidavit (kiapo)). Zechariah Wakili Msomi (zakariamaseke@gmail.com)