Maana ya Kifungo cha Maisha

Maana ya Kifungo cha Maisha

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Jamani tusaidiane

leo nimeona gazeti la Nipashe likiandika Babu Seya Kufia Jela

Je nini maana halisi ya kifungo cha maisha?
 
nijuavyo mm yani unakaa jela miaka yako yote yani utaishi huko mpaka Mungu atakapokuchukua
 
nijuavyo mm yani unakaa jela miaka yako yote yani utaishi huko mpaka Mungu atakapokuchukua
sawa na wengine watatiririka, lakn kama umesikiliza vizuri, Babu anasema wanasubiri msamaha (parole) wa Rais, ina maana yake.
 
Amavubi hyo parole inawezahusu makosa kama ya kina babuseya kweli?? Na itatolewa na rais yupi? JK ama mwingne?
 
Last edited by a moderator:
yaani maana yake utaishi gerezani maisha yako yote yaliyobaki, kama we ni papii kocha kijana mdogo tu ni kwamba utaishi jela ujana wako wote hadi uzee wako wote utakufa na utazikwa na wanajela wewe maisha yako yote ni wa jela, utakuwa mfungwa maisha yako yote ya hapa duniani.
 
mg1125.jpg
 
yaani maana yake utaishi gerezani maisha yako yote yaliyobaki, kama we ni papii kocha kijana mdogo tu ni kwamba utaishi jela ujana wako wote hadi uzee wako wote utakufa na utazikwa na wanajela wewe maisha yako yote ni wa jela, utakuwa mfungwa maisha yako yote ya hapa duniani.
umedadavua vizuri, je una rejea yoyote?
 
Kifungo cha maisha si adhabu, ni sehemu ya maisha tu, kwani hutaona tofauti ya kufungwa na kutokufungwa..adhabu ni kufunguliwa na kufungwa, kufunguliwa na kufungwa, kufunguliwa na kufungwa....

Kwamfano, adhabu ya Kifo kwa muadhibiwa si adahabu, ni adhabu kwa jamaa na ndugu zako
 
Tuendelee kuzama jamani, huenda kuna kapoint mknakamiss
 
Last edited by a moderator:

Mada nzuri Amavubi

Naomba kutanua mjadala kidogo.

Ukipitia hii case http://www.judiciary.go.tz:8081/hel...ppeal/TheRepublicVsMaryamWadud 10 OF 2010.htm

Kuna mahali wakili wa utetezi(kama alivyokuwa wakati huo) Dk. Fauz Twaib amenukuliwa aki_argue kwa maneno haya "imprisonment for life does not mean life imprisonment''
.

Embu wanasheria wasomi tusaidiane katika kuijadili mantiki yake hapa.

cc; EMT, IDUNDA, iparamasa, MAKINYA

Hiyo kesi ilikuwa inamhusu Mtanzania aliyehukumiwa kifungo cha maisha cha huko Mauritius kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo. Kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo, adhabu ya kosa alilotenda (kuingiza nchini humo gramu 223.49 za heroin) iilikuwa ni kifungo cha maisha. Kwa vile Tanzania na Mauritius zina makubaliano ya kubadilishana wafungwa, Mtanzania huyo alihamishiwa Tanzania kuendelea na kifungo chake.

Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria za Tanzania, adhabu ya kosa alilotenda ni kifungo cha miaka 20 hadi kifungo maisha. Hivyo basi akiwa Segerea, mfungwa huyo aliomba, pamoja na mambo mengine, aadhibiwe kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Mahakama Kuu ilikubaliana naye kuwa adhabu aliyokuwa anatumikia ilikuwa kinyume na sheria za Tanzania na kwamba alistahili atumikie adhabu ya kifungo cha miaka 20 tuu.

Hata hivyo, DPP alikata rufaa Mahakama ya Rufaa na ndipo basi Dr.Fauz aka-argue mbele ya Mahakama hiyo kuwa "the minimum sentence for the offence against the respondent in Mauritius is life imprisonment, whereas in Tanzania, the sentence is twenty years to life imprisonment" na kuongeza kuwa "imprisonment for life does not mean life imprisonment, hence, the least available sentence should have been imposed." Baada ya kupitia vifungu vya sheria, Mahakama ya Rufaa ikasema kuwa japokuwa mtu anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha, hicho kifungo siyo "absolute".

Ninavyoelewa, literally, kifungo cha maisha maana yake aliyekutwa na hatia atabakia gerezani kwa kipindi chote cha maisha yake au mpaka atakapopewa msamaha na Rais. Kwenye baadhi ya kesi ambazo nimesoma, sometimes unakuta judge anamhukumu mshtakiwa kifungo cha maisha na kumtaka atumikie kifungo siyo chini ya miaka fulani. Kwa hiyo, mfunguwa akishatumikia muda uliowekwa na mahakama anaweza kuomba parole pamoja na kwamba kifungo chake ni cha maisha.

Kwa upande mwingine, kuna kesi nyingine kutokana na uzito wa kosa lenyewe, judge anaweza kumhukumu mshtakiwa kifungo cha maisha na kusizitiza kuwa kifungo cha maisha anamaanisha mshtakiwa ataishi maisha yake yote gerezani bila kupewa msamaha wa aina yoyote.

Kwa hiyo, kifungo cha maisha siyo kweli ni kifungo cha maisha. Kwa, mfano Bibi Titi Mohammed alifungwa kifungo cha maisha kwa kosa la uhaini lakini akasamehewa na Rais baada ya kutumikia miaka miwili tuu. cc Amavubi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom