Maana ya maneno haya

Maana ya maneno haya

Kukamido

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
853
Reaction score
204
- Njama
- Dondoka
- Anguka

Wajuzi wa lugha naomba muongozo hapo.
 
1.Njama= Maafikiano au makubaliano au mapatano ya kufanya jambo baya dhidi ya mtu au watu wengine. Njama huweza kupangwa na mtu mmoja au zaidi dhidi ya mtu au watu wengine. 2.Dondoka= Ponyoka kutoka sehemu fulani aghalabu kitu kilipojishikiza na kutua sehemu nyingine. Mfano; embe,na chungwa KAMA VIPO KWENYE MTI. Pia mtu aliye kwenye mti akiponyoka na kutua chini huyo amedondoka. 3.Anguka= Kitendo cha kwenda chini kwa ghafla. Mfano, mtu anapoteleza au kujikwaa na kutua chini, gari linapobinuka na kulalia ubavu usio na matairi au ndege inapoporomoka kwa ghafla kutoka angani na kutua ardhini. NB; JAPO DHANA HIZI ZINAFANANA, KILA MOJA INA MAANA NA DHIMA YAKE.
 
Nashukuru sana mkuu
 
Ipi Sentensi Sahihi Kati Ya Hz, Ndege Imedondoka, Ndege Imeanguka
 
Back
Top Bottom