Maana ya maneno ya waluguru wanapomaliza kuzika

Maana ya maneno ya waluguru wanapomaliza kuzika

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Kwa sasa hata kwa baadhi ya matambiko ya kiluguru kuna maneno ya kiluguru utayasikia yanasemwa, haya maana sana ila yanaonesha hali ilivyokuwa kipindi hiko.

Kagone vigonele fungo
Munu mkulu kagona kikunza
Kwekuka wayago tokuja

Hayo maneno utayasikia kwenye matambiko, siku za hivi karibuni yamekuwa yakitamkwa na baadhi ya wasanii wa bongo muvi wanapoingiza uganga. Maneno hayo pia yametajwa na Mbaraka Mwinshehe kwenye wimbo wa Tambiko la Wahenga wimbo ambao amewataja wandewa na machifu wa kiluguru kama Mbago, Hega, Lukwele na Kingalu.

Maana ya maneno hayo

Kalale kama anavyolala fungo
Mkubwa lala ulivyojikunja
(walikuwa wanazika mtu akiwa na umbo kama yupo kwenye tumbo la uzazi)
Wewe nenda wenzako tunakula. (Ni kama kina Kibonde walivyokuwa wanasema ukifa, rafiki zako watakunywa zako bia)

Haya, Mkoba Mfuko nawaaga kwa leo, tukutane next issue kuhusu waluguru
 
Umesahau hili wakisha mzika marehemu utasikia!
Machua Machua!; Kiitikio=Ghabita!

Ninacho wapendea Waluguru wanaenda mazikoni na majembe yao, wakimaliza kuzika wanapitiliza mashambani...
 
So waluguru wanapenda kula Kama wapare na wasukuma ? Kwanini wawaze misosi tu
Hiyo ni lugha picha! yenye maana kwamba sisi tuliobaki bado tunahitaji kula;

Wewe mwenzetu huna mahitaji hayo tena!

Hivyo lazima tufanye kazi kwa bidii ili tusife na njaa...
 
Kwa sasa hata kwa baadhi ya matambiko ya kiluguru kuna maneno ya kiluguru utayasikia yanasemwa, haya maana sana ila yanaonesha hali ilivyokuwa kipindi hiko.

Kagone vigonele fungo
Munu mkulu kagona kikunza
Kwekuka wayago tokuja

Hayo maneno utayasikia kwenye matambiko, siku za hivi karibuni yamekuwa yakitamkwa na baadhi ya wasanii wa bongo muvi wanapoingiza uganga. Maneno hayo pia yametajwa na Mbaraka Mwinshehe kwenye wimbo wa Tambiko la Wahenga wimbo ambao amewataja wandewa na machifu wa kiluguru kama Mbago, Hega, Lukwele na Kingalu.

Maana ya maneno hayo

Kalale kama anavyolala fungo
Mkubwa lala ulivyojikunja
(walikuwa wanazika mtu akiwa na umbo kama yupo kwenye tumbo la uzazi)
Wewe nenda wenzako tunakula. (Ni kama kina Kibonde walivyokuwa wanasema ukifa, rafiki zako watakunywa zako bia)

Haya, Mkoba Mfuko nawaaga kwa leo, tukutane next issue kuhusu waluguru

Haya maneno yanashabihiana kwa kiasi fulani na kihehe/kibena.
 
Haya maneno yanashabihiana kwa kiasi fulani na kihehe/kibena.
Wahehe na wabena wamewahi kuishi na waluguru na ndio sababu kuna ukoo wa Wabena (Mwanaume Mbena, Mwanamke Kibena) wametokana na muingiliano huo, pia kuna ukoo wa Wahehe, ambao ni muingiliano kati yao na wahehe
 
Umesahau hili wakisha mzika marehemu utasikia!
Machua Machua!;...
Zamani maombolezo yalichukua siku nyingi, wafiwa hawakufanya kazi, kazi zilifanywa na watani. Ila siku hizi mambo ni mengi. Mathalani Mgeta ukizimia wanaweza kukuzika, hawasubiri sana
 
Back
Top Bottom