Black hermit
JF-Expert Member
- Mar 20, 2017
- 658
- 951
Wataalamu naomba msaada maana ya neno ufundi mchundo
========
Mkandarasi ni fundi mwenye taaluma ya juu kuliko mafundi wengine wa ujenzi wakiwemo wakandarasi wa barabara wanaofahamu vitu na vipimo vyote vitakavyotumika katika ujenzi husika. Mkandarasi hufanya kazi maalumu zikiwemo za ujenzi na ugavi wa vifaa, kwa mkataba maalumu, kwa muda maalumu, na kwa malipo maalumu. Mara nyingi mkandarasi anakuwa na kampuni kubwa kubwa, maana yake yeye analisimamia hilo jengo kuanzia chini mpaka juu ujenzi wake, mkandarasi hadhi yake ipo juu zaidi.
Mkandarasi ni tofauti na fundi ujenzi na mara nyingi wakandarasi hawafanyi kazi kama mtu mmoja mmoja. Fundi ujenzi ni mtu anayeshughulika na ujenzi wa nyumba za kawaida tu.
Fundi stadi ni fundi ujenzi mwenye ujuzi na utaalamu wa kupima jengo na kuanza kulijenga mwanzo hadi mwisho. Kwa sababu anayo taaluma hiyo, anao utaalamu na anaweza kuifanya kazi hiyo vizuri yeye akiwa kama msimamizi, tunamuita fundi stadi kwa sababu ana uwezo wa kuifanya kazi bila kusimamiwa na mtu mwingine
Fundi Mchundo: Ni yule anayefanya kazi chini ya uangalizi wa fundi stadi. Huyu ni fundi mchundo kwa sababu bado anaendelea kujifunza na kuelekezwa kutoka kwa fundi mwenye utaalamu zaidi ya huyu ambaye ni fundi stadi
Fundi Muashi: Huyu ni mtu ambaye ujuzi wake ni wa kujenga nyumba kwa kutumia mawe au tofali, muashi ni tofauti na mkandarasi. Mkandarasi yeye anakuwa mkandarasi wa barabara, mkandarasi wa madaraja, mkandarasi wa ghorofa, mkandarasi wa mitambo mbalimbali, mkandarasi haishii kwenye ujenzi tu, hata kule kusambaza vifaa ili ni dhamana ya mkandarasi.
Kupaua ni kupigilia mbao au miti juu ya kuta za nyumba.
Kuezeka ni kupigilia mabati, kuweka vigae, makuti au nyasi juu ya paa la nyumba.