Hata mimi jana nimeota nakula samaki mbichi maeneo ya sokoni alafu baada ya hapo ikafata ndoto nyingine ambapo marafiki zangu niliosoma nao(huyo mmoja ni marehemu kwa sasa) walikuwa wakinifurahia mimi baada ya kupotezana tangu shule ya msingi, ghafla katika kunifurahia wakaanza kugombana mara nikawaona mmoja ana lirungu lililochongoka na mwingine ameshika panga lililochongoka, sasa kwa ile style waliyokuwa wameshikana mashati wakachomana kifuani.
Yaani mmoja akamsukumizia mwenzake panga kifuani na mwingine akamsukumizia mwenzake rungu kifuani.
Sikudhubutu kuendelea kuangalia maana yule ambaye ni marehemu ndio alichokozwa na ndio niliona ameshamzamishia mwenzake panga kwenye moyo likazama na damu zikarudi hatari huku huyu mwingine nae akijitahidi kumzukumizia mwenzake rungu kwenye moyo pia ila sikuona rungu likimchoma huyu mwingine ila niliona likikaribia kumchoma.
Ile ndoto ilinishtua na nikaamka nikiwa nimechoka
Hao wote walikuwa ni marafiki wakubwa darasani na nilikuwa rafiki yao mkubwa pia.
Alafu huyu ambaye ni marehemu kwa sasa, kuna mdogo wake ambae ni rafikiangu sana hapa mjini na hata leo nimeenda kumsalimia sijamkuta ofisini kwake nikaambiwa ameenda kunywa chai.
Huyu mwingine aliyechomwa na panga kwenye moyo yupo hapahapa mjini ila hatuna mawasiliano tangu tulipomaliza shule ya msingi