Tetesi: Maana ya Ndoto kuhusu samaki

Kingdom78

Member
Joined
May 31, 2015
Posts
72
Reaction score
77
habari wapendwa katika Imani nimepitia baadhi ya vitabu ambavyo nimeandikwa kuhusu ndoto, Na vitabu vingi vimeandika samaki maana yake ni watu. na ukiota unavua samaki maana yake unapeleka kondoo kwa bwana.


sasa swali langu na ukiota unakula Samaki hii inamaanisha nini?

Nawasilisha [emoji120]
 
Hata mimi jana nimeota nakula samaki mbichi maeneo ya sokoni alafu baada ya hapo ikafata ndoto nyingine ambapo marafiki zangu niliosoma nao(huyo mmoja ni marehemu kwa sasa) walikuwa wakinifurahia mimi baada ya kupotezana tangu shule ya msingi, ghafla katika kunifurahia wakaanza kugombana mara nikawaona mmoja ana lirungu lililochongoka na mwingine ameshika panga lililochongoka, sasa kwa ile style waliyokuwa wameshikana mashati wakachomana kifuani.
Yaani mmoja akamsukumizia mwenzake panga kifuani na mwingine akamsukumizia mwenzake rungu kifuani.
Sikudhubutu kuendelea kuangalia maana yule ambaye ni marehemu ndio alichokozwa na ndio niliona ameshamzamishia mwenzake panga kwenye moyo likazama na damu zikarudi hatari huku huyu mwingine nae akijitahidi kumzukumizia mwenzake rungu kwenye moyo pia ila sikuona rungu likimchoma huyu mwingine ila niliona likikaribia kumchoma.
Ile ndoto ilinishtua na nikaamka nikiwa nimechoka

Hao wote walikuwa ni marafiki wakubwa darasani na nilikuwa rafiki yao mkubwa pia.
Alafu huyu ambaye ni marehemu kwa sasa, kuna mdogo wake ambae ni rafikiangu sana hapa mjini na hata leo nimeenda kumsalimia sijamkuta ofisini kwake nikaambiwa ameenda kunywa chai.
Huyu mwingine aliyechomwa na panga kwenye moyo yupo hapahapa mjini ila hatuna mawasiliano tangu tulipomaliza shule ya msingi
 
tuwasubiri wataalamu wa ndoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…