Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tafakuri jadidi:
Neno jadidi asili yake ni upya au mpya, hivyo ukisema "tafakuri jadidi" maana yake itakuwa ni fikra mpya. (au maana inayofanana na hiyo).
Upembuzi Yakinifu:
Upembuzi ni kuchambua. ...Yakinifu asili ya neno yakinifu limetokana na neno yakini ambayo tafsiri yake ya harakaharaka ni uhakika.
Hivyo tunapata maana ya "upembuzi yakinifu" ni uchambuaji (wa masuala) kwa umakini. (au maana inayoshabihiana na hilo).
OBS mimi si mtaalamu wa lugha ya Kiswahili.
Nimepatwa kuulizwa swali humu kuhusu haya maneno
- Tafakuri tunduizi
- Tafakuri jadidi
- Upembuzi yakinifu
Tusaidiane kwa kina wadau wa lugha