Maandalizi ya kubinafsisha Bandari yalikuwa makubwa, sasa ni reli

Maandalizi ya kubinafsisha Bandari yalikuwa makubwa, sasa ni reli

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
866
Reaction score
625
Mheshimiwa Posi nimekusikiliza vizuri kipindi cha jambo na nimesoma citizen ninakukupa maua yako toka nyota yako ilipong'ara serikali ya awamu ya Tano umefaa kila kona uliyopelekwa kutumikia Taifa, naamini unaweza kuishauri serikali ikakusikia kama mwana uchumi.

Hivi inaingia akilini kweli kuprivetize reli, tofauti na kelele za bandari iko wapi, umekaa Nchi za ulaya Uingereza walijaribu lakini wakastuka wameirudisha kuwa owned na serikali, hatuoni kwamba tunaweza kuwa tunashauriwa vibaya?

Tumeweka trillioni nyingi sana wajukuu na vitukuu watalipa, kweli tumpe mtu aweke wawagon yake akiamua sibebi pamba yetu mtasemaje na mmeingia mkataba.

Hili nalo lisipelekwe mzobemzobe tutaumizwa huko mbele, serikali inashindwa nini kuendesha hata reli tu jamani, natamani Nyerere afufuke.

Reli ya uhuru tumeitelekeza watu binafisi watumie maloli mabarabara yanayojengwa na jasho la mtu mnyonge zinaharibika kabla ya wakatiwake na faida kubwa nikwa wachache.
 
Back
Top Bottom