Maandalizi ya Mkoa mpya wa Chato, Buchosa wakubali kuhamia Geita

Maandalizi ya Mkoa mpya wa Chato, Buchosa wakubali kuhamia Geita

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Katika kile kinachoonekana ni maandalizi ya kuanzishwa na kutangazwa kwa mkoa mpya wa Chato, Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa wamekubali kuhamia mkoa wa Geita.

Wananchi wa Buchosa wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma Mwanza wakati wapo karibu na mkoa wa Geita.

Inasadikika chini ya kapeti, Tarehe 14/10/2021 siku ya Nyerere na kilele cha mbio za mwenge kitaifa, mkoa mpya wa Chato utatangazwa!

DDAE8707-C225-4B18-91F2-F0F4BDA2364F.jpeg
 
Na sisi wa ulanga vipi!? Mbona mnatuacha ua kwakua hatujatoa mkuu wa nchi!?
Kweli kabisa,Morogoro ni Mkoa mkubwa sana sia ajabu mtu akatoka Morogoro mjini kufika huko anatumia siku nzima akiwa safarini,ni kuwapa tabu wananchi tu kuzifuata huduma umbali mrefu
 
Mbona tunalazimisha Mambo? Taarifa nilizo nazo ni kwamba watu wa Ngara hawataki kuingizwa kwenye mkoa mpya wa Chato isipokuwa tu Kama makao makuu ya mkoa huo mpya yatakuwa Biharamulo.
 
Katika kile kinachoonekana ni maandalizi ya kuanzishwa na kutangazwa kwa mkoa mpya wa Chato, Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa wamekubali kuhamia mkoa wa Geita.

Wananchi wa Buchosa wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma Mwanza wakati wapo karibu na mkoa wa Geita.

Inasadikika chini ya kapeti, Tarehe 14/10/2021 siku ya Nyerere na kilele cha mbio za mwenge kitaifa, mkoa mpya wa Chato utatangazwa!

View attachment 1957987
Kutakuwa na mkuu wa mkoa,wilaya na wakurugenzi,hivi hawaoni gharama kuongezeka au tozo itasaidia?Hiyo Geita yenyewe bado japo ni mkoa.CCM linapokuja suala la masirahi yao hawaogopi gharama hata iwe kubwa vipi.Natabiri sasa kila mkoa utataka uwe na viongozi wa juu serikalini na hapo ndipo taifa linaelekea kumeguka.Ile kauli yao kuwa usione vyaelea vimeundwa wameacha kuu-ishi.
 
Mkoa wa Kigoma unaundwa na wilaya kongwe nne ambazo ni Kigoma Uvinza Kasulu na Kibondo. Wilaya zote hizo zinatumia lugha ya kiha na mila na tamaduni zake zimo kwenye mpaka wa mkoa w Kigoma ambazo zimekuwepo hata kabla ya uhuru.

Mpango uliopo wa kuumega mkoa wa Kigoma hususan wilaya ya Kakonko kwenda kuunda mkoa wa Chato ni batili na haukubaliki. Natoa rai kwa mheshimiwa Rais asikubali kuunda mkoa mpya kwa kuvunja mkoa mwingine kwa maslahi binafsi ya watu au kundi fulani.

Kuna uwezekano wa kutengeneza mgogoro kama ule uliopo Ziwa Nyassa kati ya Tanzania na Malawi .... Mipaka ya mikoa iliyopo iheshimiwe.
 
Back
Top Bottom