Maandalizi ya mkutano wa wafanyabiashara wa mifugo, kilimo wa tanzania na comoro yakamilika

Maandalizi ya mkutano wa wafanyabiashara wa mifugo, kilimo wa tanzania na comoro yakamilika

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Maandalizi ya Mkutano wa Wafanyabiashara wa Mifugo, Kilimo wa Tanzania na Comoro yakamilika

Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Saidi Yakubu, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jumuiya ya Wakulima, Wavuvi na Sanaa wa Comoro Mhe. Abdillah M’Saidie ambaye amemueleza kuwa wamekamilisha maandalizi yote muhimu ya Kongamano la Kilimo, Mifugo na Usafirishaji kati ya Wafanyabiashara wa nchi hizo mbili.

Awali Balozi Yakubu alimueleza Bwana M’Saidie kuwa takriban wafanyabiashara 45 na Maafisa Waandamizi Watano wa Tanzania wanatarajia kushiriki na baadhi wamekwishafika Comoro hivyo kutoa wito kwa Wafanyabiashara wa Comoro kushiriiki kwa wingi ili kuongeza vyanzo vyao vya upatikanaji wa bidhaa za Kilimo na Mifugo.

IMG-20240819-WA0016.jpg

Kwa upande wake Bwana M’Saidie alieambatana na uongozi wa Jumuiya hiyo alimuarifu Balozi Yakubu kuwa maandalizi kwa upande wao yamekamilika na wameainisha mahitaji ya msingi ya mazingatio kwa wenzao wa Tanzania na matumaini yao ni kuwa Kongamano hilo litafungua ukurasa mpya wa ushirikiano baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano baina ya Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro, Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) na Jukwaa la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Jumuiya ya Wafugaji, Wavuvi na Sanaa Comoro na Mamlaka ya Uwekezaji Comoro.

Katika kongamano hilo wafanyabiashara wa Tanzania watapata kuelezwa mambo muhimu ya kuzingatia katika kufanya biashara Comoro, fursa zilizopo na maeneo ya uwekezaji yaliyopo na litafanyika Jumatano tarehe 21 Agosti, 2024 na kufunguliwa na Gavana wa Kisiwa cha Ngazija, Mhe. Ibrahim MZE.
IMG-20240819-WA0017.jpg
 

Attachments

  • IMG-20240819-WA0018.jpg
    IMG-20240819-WA0018.jpg
    104.7 KB · Views: 10
  • IMG-20240819-WA0019.jpg
    IMG-20240819-WA0019.jpg
    268.7 KB · Views: 11
  • IMG-20240819-WA0015.jpg
    IMG-20240819-WA0015.jpg
    221.8 KB · Views: 11
Back
Top Bottom