Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #21
Kichuguu,Maandamano hayo hayakuwa na msingi wowote bali yalikuwa ni chanzo tu cha kuchochea hasira za kisiasa kupitia dini kwani ilitakiwa ijulikane wazi kwa waislamu wote kuwa maoni ya Sofia kwenye UWT hawawezi kubadilisha msaafu unaotumiwa duniani pote. Yalichangia kuonyesha sense of insecurity kwa wafuasi wa dini hiyo.
Sasa mzee mwenzagu nawe unaamini kweli kuwa maneno ya Sofia yangeweza kubadilisha msaafu.?Kichuguu,
Naelewa kwa nini kwako unaona kauli ile ni nyepesi.
Wala sikulaumu.
Geb,Elimu duni kwa waislam ni janga Sana kwa dunia iliyostaarabika.
Kichuguu,Sasa mzee mwenzagu nawe unaamini kweli kuwa maneno ya Sofia yangeweza kubadilisha msaafu.?
Tuliokulia vichochoroni tunaamini kuwa kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba kupapa usingizi, au kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji. Kwa nini hawakuona kuwa hizo ama zilikuwa kelele za mlango au ni kelele za chura tu wakaendelea na shughuli zao kuliko kuanza kufanya vurugu?
Kichuguu,
Yasingeweza kubadili chochote.
Walichochelea Waislam kitendo chake kingefungua mlango wa kuichezea Qur'an.
Baada ya siku ile hali imetulia hadi leo.
Somo limesomeka na kueleweka.
Biti...Hakika Sheikh Mohammed wao wanaona ni maneno mepesi aliyosema Sofia lakini kwetu sisi Waislamu tuliona kama ni dhihaka ya kiwango cha juu. Leo yeye alianzisha lile na kesho yake angekuja mwingine kusema makubwa zaidi.
Kipande kipi hicho mkuuUmeacha kipande muhimu sana...
Kipande kipi hicho mkuu
Rodrick,Dini ni imani, kauli ya Sophia Kawawa ambaye pia ni mwislam iligusa imani ya waislam wenzake na inawezekana aliitoa sababu yeye alikuwa mwathirika kwani mmewe ambaye pia alikuwa ni mwislam alioa mke zaidi ya mmoja na yeye akiwa mke mkubwa.
Kauli za mashehe kukemea kauli yake zilikuwa sahihi na hata kuandamana pia ilikuwa sahihi ila kushambulia maofisi inaonyesha kulikuwa na ajenda nyingine iliyojificha
Hilo la vurugu ni kawaida hasa kwa vijana ambao huwa wanaona sifa kufanya vitendo viovu kama vile kuvunja maduka na kuiba vitu, kupiga mawe ovyo, na kadhalika. Na hii hutokea sehemu nyingi duniani na hasa pale polisi wasipokuwepo katika eneo la tukio.Dini ni imani, kauli ya Sophia Kawawa ambaye pia ni mwislam iligusa imani ya waislam wenzake na inawezekana aliitoa sababu yeye alikuwa mwathirika kwani mmewe ambaye pia alikuwa ni mwislam alioa mke zaidi ya mmoja na yeye akiwa mke mkubwa.
Kauli za mashehe kukemea kauli yake zilikuwa sahihi na hata kuandamana pia ilikuwa sahihi ila kushambulia maofisi inaonyesha kulikuwa na ajenda nyingine iliyojificha
Kumbe huyu mama alishawahi kuolewa na Kawawa?
Ni mke wa Pius Msekwa kwa sasa huyu nadhani!
hilo lakujisaidia haja ndogo na maji tlilika nakupinga mbona wengi nawaona hata vichakani wanaenda bila majiGeb,
Kwa asiyekuwa Muislam atapata tabu sana kuelewa kwa nini Muislam anapokwenda haja kubwa au ndogo lazima ajikoshe kwa maji tena yanayotiririka.
Halikadhalika atapata tabu kujua kwa nini anaposwali lazima atawadhe kuchukua udhu.
Hivyo hivyo asiyekuwa Muislam hawezi kuelewa kwa nini ilipoguswa Qur'an mara moja na bila kuchelewa Sheikh Ali Ani, Sheikh Nasser Bachu na masheikh wengine walitoa matamko ya tahadhari.
Qur'an ni kauli yake mwenyewe Allah SW.
Ningeweza kueleza mengi lakini naamini nimeeleweka.
Ndiku...hilo lakujisaidia haja ndogo na maji tlilika nakupinga mbona wengi nawaona hata vichakani wanaenda bila maji
Sofia Kawawa.Mwanamke alitetea wanawake wenzake kwa kusema kitabu kinachowakandamiza kibadilishwe
Mwanaume huko zanzibar Ambaye kitabu kinampa pawa ya kukandamiza wanawake akaamua kuchochea maandamano .
Ni kweli hicho kitabu kinawakandamiza wanawake
Badala ya wanaume kujibu hoja wakaandamana ili waendelee kutetea kitabu kinachowapa pawa ya kuwakandamiza wanawake.
Swali kwa mtu mwerevu mwenye busara na aliye neutral(asiye na upande)
Nani alikuwa hero kwenye hii story?