Nimetaarifiwa kuwa kuna maandamano ya amani ya watu kiasi cha 200 mpaka 300 aykitokea Haile Saleisi kuelekea Ocean Road yamesababisha magari yasiende, kuna mtu ana taarifa yanahusu nini haya maandamano
Kama ni haya yaliyoanzia Kinondoni Road basi ni maandamano ya amani ya waislam ya Mwaka mpya wa kiislam ambao umeanza leo. Tatizo ni nchi yetu tu, vyombo vya dola havina kawaida ya kuwapasha habari watumiaji barabara lakini maandamano hayo yalikuwa na kibali na wana-usalama walikuwepo kuongoza haya maandamamno ambayo yalitanguliwa na dhifa pale Kinondoni Muslim ofisi za BAKWATA