Maandamano Kenya na hatari ya usalama wa nchi yetu

Maandamano Kenya na hatari ya usalama wa nchi yetu

Kiungopunda

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2023
Posts
1,349
Reaction score
3,145
Kwa hiki kinachoendelea Kenya na kinachofanywa na vijana dhidi ya ongezeko la gharama za maisha ni tahadhari kwa viongozo waliopo madarakani nchini mwetu.

Kawaida, mwanadamu yeyote ana kiwango cha uvumilivu hususani pale anapokosa uhakika wa Kesho tonana na ugumu wa maisha, kukosa ajira, ufisadi unaopitiliza, dharau toka kwa watalawala n.k.

Kwa yanayotokea Kenya kwa vijana wasio na ajira, maboda boda, mama mboga n.k kuingia mitaani yalianza kama kupinga mswada wa fedha ila sasa yanaenda kugeuka kwani vijana hao wameingia bungeni, kufanya vurugu na kuharibu mali za Bunge.

1719330098882.jpg

Sio kama vijana wa Kenya wana uwezo au ujasiri kuliko vijana wa Tanzania, ila wao wamechoka tokana na kukosa ajira, kukandamizwa na viongozi na vyombo vya usalama. Hawaoni uhaueni kwenye maisha yao ya kila siku.

Movement kama hii ilipita ukanda wa Kaskazini ya Afrika. Ilisababisha kudondoka kwa Serikali zilizokuwa zinaongozwa kwa mkono wa chuma kwani hakuna dola iliyowahi ishinda nguvu ya umma.

Hata nchini kwetu, kuna idadi kubwa ya vijana wasio na ajira, machinga, boda boda pamoja na wale waliokuwa JKT ambao hawana ajira na wapo mitaani. Vijana hawa ni bomu kubwa na serikali ya Tanzania inatakiwa iwahandle kwa umakini kwani kwa yanayoendelea Kenya, kunahitajika moto kidogo tu kuanzisha movement hiyo hapa Tanzania. Hiki pia tukionacho kwa wafanyabiashara walioanzisha mgomo nchi nzima sio cha kwenda nacho kwa kejeli, ubabe na kutishana.

Kwa movement ya Kenya, natoa Rai kwa serikali yetu kwenda kwa hekima katika aina yoyote ya mgomo ukiwemo wa wafanyabiashara na hawa viongozi wapuuzi akina Chalamila wanatakiwa wawekwe mbali na hii migomo. Nawasihi viongozi, msidanganyike na kutishia kupeleka majeshi kutishia wagomaji wakiwemo wafanyabiashara kama alivyofanya Yule mwehu Chalamila kwani hakuna Jeshi chini ya mbingu linaloishinda nguvu ya umma.

Kwa hiki cha Kenya, hata sasa Ruto na viongozi wengine hawahamini kama yamefikia hapa. Walidhani mzaha na wabunge kusema wamehongwa ila leo wamepata cha moto.
1719330090222.jpg

Najua, JF ina watu wengi waliopo ndani ya system yetu, nendeni taratibu na migomo yoyote sasa hata huo wa wafanyabiashara, mkidharau nanyi mtarudi kizimkazi kwa kupiga mbizi baharini.

Nashauri, naipenda nchi yangu. Mungu ibariki Tanzaia Mama yangu.
 
Viongozi wa Africa wanaishi maisha ya kufuru na starehe za juu wakilipana maposho na mishahara na kujilimbikizia mali huku wananchi wakifa njaa.Tanzania,Tanzania, Tanzania nimekuita mara 3!
 
Shida ya viongozi wengi waliopo madarakani hawana element za leadership,, hawajasomea but the big issue ni kuomba kuwa na amani nchini, machafuko yanarudisha maendeleo nyuma
 
Back
Top Bottom