Mfikirishi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 8,939
- 10,403
Binadamu ni akili inayoishi ndani ya mwili! Na akili inahitaji elimu bora ili kuikomaza vizuri. Siasa na serikali ni mifumo ya kijanja janja sana. Inahitajika akili iliyokomaa kuweza kukabiliana nayo!
Maandamano yanayofanyika nchini Kenya hayana viongozi wa kisiasa! Ni vijana walioelimisha akili zao lakini mifumo ya wanasiasa imewatelekeza! Adui yao mkubwa ni wanasiasa na mifumo yao kandamizi! Wamekata tamaa! Hawana cha kupoteza! Wapo tayari kutafuta wanachokitaka!
Tunaweza kuwadharau kwa sababu zozote zile lakini vijana wa Kenya wanazidi kutu-prove wrong! Ndiyo! Wana ukomavu wa akili! Ndicho pekee unachoweza kusema. Najua wale wa "sisi tunataka amani" hawatanielewa!
Pia soma:Nguvu ya Umma: Bunge lalazimika kubadilisha Muswada wa Sheria ya Fedha baada ya maandamano ya Wananchi