Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Uhuru Kenyatta
Rais wa mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametoa tamko kuhusu maandamano yanayoendelea dhidi ya Muswada wa Fedha.
Kiongozi huyo wa zamani wa taifa alituma salamu zake za rambirambi kwa Wakenya waliopoteza maisha yao wakati wa maandamano ya Jumanne, akisema ilikuwa haki yao ya kikatiba kuandamana.
"Nawajia nikiwa na moyo mzito nikiwa na huzuni kwa kupoteza maisha kutokana na hali ya sasa inayotawala nchini. Ni haki ya Wakenya kuandamana kama inavyotambuliwa na Katiba ya Kenya 2010. Pia ni jukumu la viongozi kuwasikiliza wale wanaowaongoza," alisema Uhuru.
Uhuru aliendelea kuwataka wananchi kuwa watulivu na kuhimiza viongozi wakumbatie mazungumzo na watu.
"Kama rais wenu wa zamani, nimehisi uzito wa kuwaongoza Wakenya. Kwa hivyo naomba hekima na ustaarabu vianzishwe na amani na maendeleo yawe mali yetu sote kama watoto wa Kenya," alisema.
Rais huyo wa zamani alithibitisha uungaji mkono wake kwa Wakenya na kuwataka viongozi "Waongee na watu na si kwa watu."
"Ninaomba amani na uelewa kwa kila Mkenya na kwa sote tukumbuke kuwa Kenya ni kubwa kuliko mmoja wetu; hakuna kitu kilichochongwa kwenye jiwe ambacho hakiwezi kubadilishwa," alisema.
PIA SOMA
- LIVE - Yanayojiri Maandamano Kenya: Waandamanaji wafika Bungeni, wawili wauawa kwa risasi
- Waandamanaji Nairobi wavamia jengo la Bunge baada ya kuwashinda nguvu polisi, yasemwa waandamanaji 10 wameuawa kwa kupigwa risasi halisi