Maandamano kwa JK yapigwa marufuku

Maandamano kwa JK yapigwa marufuku

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Imetolewa mara ya mwisho: 24.10.2008 0057 EAT

• Maandamano kwa JK yapigwa marufuku

Na Rehema Mwakasese

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema haliko tayari kutoa kibali cha maandamano ya vuguvugu la kudai mabadiliko ya Katiba ikiwamo kumpunguzia Rais madaraka na kufutwa adhabu ya kifo.

Akizungumza jana na gazeti hili, Kamishna Msaidizi wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Evarist Mangala, alisema Jeshi hilo halitatoa kibali kwa waaandaaji wa maandamano hayo kwa sababu Rais hayupo tayari kuyapokea.

Bw. Mangala alisema waandaaji hao walikwenda ofisini kwake juzi kuomba kibali hicho, lakini hawakuwa na kielelezo chochote ambacho kinaonesha Rais alikwishawakubalia kuyapokea.

"Walikuja hapa ofisini juzi na tukaongea nao na nilipotaka vielelezo vinavyoeleza Rais kuyapokea maandamano hayo hawakuwa navyo na pia hawakuwa na maelezo yoyote ambayo yanaonesha Rais kukubali. Kwa hiyo tukaona hakuna umuhimu wa kutoa kibali cha maandamano hayo," alisema Bw. Mangala

Alisema kuwa endapo wanaharakati hao wataandamana bila kibali, sheria itachukua mkondo wake kwani watakuwa wamevunja taratibu za nchi, hivyo aliwataka wasifanye maandamano hayo.

Maandamano hayo ambayo yamepewa jina la Mkusanyiko Mtakatifu wa Amani (MMA) yatashirikisha wananchi wa kawaida na wanaharakati ambapo hoja nyingine wanazotaka zitekelezwe ni pamoja na kutaka kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi na sheria za uchaguzi ziangaliwe upya ili haki itendeke.

Pia wanataka Umoja wa Mataifa usaidie kuwafikisha mahakamani watu waliohusika na mauaji kisiwani Pemba Januari 27, 2001 ikiwa ni pamoja na waliofanikisha mauaji hayo bila kuzingatia haki za binadamu, yakiwamo ya Bulyanhulu, Shinyanga.
 
Nani kawaambia kinahitajika Kibali?

Tatizo wakati mwingine ni sisi. Wao kwanza kwa nini walienda ofisini kwa huyo bwana? Kinachotakiwa ni kutoa taarifa kwamba siku fulani na saa fulani tutaandamana kupitia njia fulani ili polisi wawe na taarifa na ikibidi watoe ulinzi. Sasa wao kilichowapeleka kwa huyo kamanda ni nini kama sio ushambenga?
 
Tatizo wakati mwingine ni sisi. Wao kwanza kwa nini walienda ofisini kwa huyo bwana? Kinachotakiwa ni kutoa taarifa kwamba siku fulani na saa fulani tutaandamana kupitia njia fulani ili polisi wawe na taarifa na ikibidi watoe ulinzi. Sasa wao kilichowapeleka kwa huyo kamanda ni nini kama sio ushambenga?

Nani na lini aliandamana bila kibali cha polisi nchini Tanzania?
 
The notion that Tanzania is a free country with adequate, if not impeccable, civil liberties is blown away by such ignorant civil servants.

The people have a right to demonstrate to Ikulu whether the president will OK that or not, the entire point of the demonstration is to put pressure on the president, so asking the president to be the approver of a system that will put him in check is the epitomy of cronyism, if not dadaism.
 
Hii sasa vurugu kila mtu akiamka asubuhi anatangaza maandamano!
 
Back
Top Bottom