EDWIN BAJUNGU
New Member
- Jun 8, 2020
- 4
- 3
Sisi hatujui sheria lakini pale kijiweni kwetu kulitokea ubishi baina yetu tukibishana kuwa maandamano na mikutano inayofanywa na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema Tundu Lissu wakati anapita mikoa mbalimbali kutafuta wadhamini kama ni ukiukaji au siyo ukiukaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.
Baadhi yetu tulisema ndiyo ni ukiukaji wa sheria na kanuni za uchaguzi. Na wengine tulisema Hapana siyo ukiukaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.
Katika makundi haya mawili, kila kundi lilitoa hoja zake kutetea msimamo wake. Japo sidhani kama kuna kundi lililotoa hoja zenye mashiko ya kisheria kwani wote tuliokuwa tunabishana hakuna aliyesomea sheria.
Nadhani msingi wa mabishano yetu ulikuwa ni ushabiki tu kila kundi likishabikia na kutetea upande wa chama linachokipenda. Ubishi ulianza baada ya mmoja wetu kutusomea ujumbe aliyotumiwa katika simu yake ulioeleza kuwa Lisu anaweza kukatwa na kuondolewa na Tume ya uchaguzi kwa kosa la kuanza kampeni mapema kabla ya kuruhusiwa rasmi na Tume ya uchaguzi.
Upande uliokuwa unadai kuwa Lissu amekiuka sheria na kanuni za uchaguzi, ulisisitiza kuwa Lissu lazima akatwe na kuenguliwa na Tume ya uchaguzi katika mbio za kugombea urais kwa kosa la kufanya kampeni mapema kabla ya kuruhusiwa rasmi na Tume ya uchaguzi.
Lakini upande uliokuwa unadai kuwa Lisu hajavunja sheria wala kanuni za uchaguzi. Kundi hilo lilisisitiza kuwa Lisu alikwenda mikoani kutafuta wadhamini.
Lakini kwa kuwa wanachama wa Chadema wamejitokeza kwa wingi kumdhamini Lisu maadui wa chadema na Lisu wanaona wivu na kuanza kudai kuwa Lisu amekiuka sheria na kanuni za uchaguzi.
Ukiwa kama mtu makini unayeamua kwa haki, Je, ni kundi lipi liko sahihi? Je ni kundi linalodai kuwa Lisu amevunja sheria na kanuni za uchaguzi au kundi linalodai kuwa Lisu hajakiuka sheria wala kanuni za uchaguzi?