Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Sijui kwanini sisiemu wanaikana sera yao penzi ya ubinafsishaji na hata kudiriki kujigamba kwenye mikutano yao bandari haziuzwi wala hazibinafsishwi wakati wamebinafsisha.
Kama wapinzani wameshindwa kitu kidogo kama kulinda kura wataweza kuongoza maandamano na kuwang'oa watawala?
Ukweli ni kuwa hawawezi. Ubinafsishaji ni suala la kisera siyo la kisheria na Mahakama Kuu ilijichanganya kwa kuoni vinginevyo na ndiyo maana uamuzi wao una mapungufu mengi ya kisheria ambayo mahakama ya rufani itayarekibisha bila kuathiri azimio la kibunge la kuwamilikisha waarabu wa Dubai bandari zetu.
Wapinzani wajikite kwenye kubuni mikakati ya kulinda kura badala ya kupoteza nguvu kwenye utekelezaji wa sera za ubinafsishaji za chama tawala.
Kama wapigakura wamekerwa na sera hizo basi waonyeshe kwenye vituo vya kura kwa kuikataa sisiemu na kuzilinda kura zao bila kuwaruhusu makada wa sisiemu kuendelea kuwachagulia viongozi ambao siyo chaguo lao.
Kama huwezi kubuni mikakati ya kuwadhibiti wakurugenzi wa majiji na halmashauri (ambao ndiyo makada wa sisiemu na wamebandikwa hapo kwa kazi moja tu ya kukuibia kura yako) kupindisha haki yako ya mpigakura basi endelea kuwaacha wauze kila kitu na kuna siku hata wewe watakuweka sokoni na utabinafsishwa au hata kuuzwa kwa anayekuhitaji kwa kuzubaa zubaa kwako
Ukweli