MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 305
- 728
Na Mwandishi Wetu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kina mpango wa kufanya maandamano yasiyo halali Jijini Dar es salaam katika siku za karibuni ambapo kulingana na maelezo ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, maandamano hayo ni kwa ajili ya kupinga vitendo vya utekaji nyara na mauaji ya watu kadhaa, ambayo Mbowe na wanasiasa wengine pamoja na wanaharakati wanadai vinafanywa na Serikali.
Lakini mara kadhaa Serikali kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wasaidizi wake wamesema bayana Serikali haihusiki si kwa ndewe wala sikio.
Ndiyo maana Rais Samia alikemea vitendo hivyo na kuviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio hayo yanayoleta taharuki nchini.
Siyo hivyo tu, bali hata chama tawala CCM kimetoka hadharani na kukemea vitendo hivyo visivyo vya kiutu. Lakini katika hali ambayo inaonyesha kwamba ni mbinu ya wapinzani kutafuta "kiki", Chadema kimeamua kuhamasisha maandamano kupinga mauaji hayo.
Serikali imekwishatoa tahadhari kwamba maandamano hayo yasifanyike, lakini ajabu ni kwamba Chadema wanaonekana wanalazimisha yafanyike huku wakiungwa mkono na wanaharakati.
Kwanza wananchi wanapaswa kutii katazo la Serikali la kutoandamana kwa sababu wanatumiwa na wanaharakati wa kisiasa kama ngazi yao ya kufanikisha mambo yao.
Pili, hii siyo mara ya kwanza kwa CHADEMA wanaharakati wa kisiasa kukaidia amri ya Serikali ya kutoandamana na matokeo yake vyombo vya Dola vinapochukua hatua stakihi wanaoumia ni wananchi huku wahamasishaji wa maandamano wakijificha.
Kimsingi, maandamano hayo yanalenga kuvuruga amani na utulivu nchini kwa sababu yanabeba agenda ambayo hata Serikali yenyewe inaendelea kuifanyia kazi kuhusu hao watekaji na wauaji wasiojulikana.
Watanzania wanapaswa kujikumbusha kilichotokea kwa jirani zao Wakenya wakati wa maandamano ya Generation Z, ambayo yameacha makovu kwa jamii ya watu wa nchi hiyo.Ni ajabu kwamba viongozi wa ChHADEMA na wanaharakati wanatolea mfano maandamano hayo ya Wakenya na kuwaita Watanzania "waoga" eti kwa kutii amri ya kutoandamana.
Kwamba, wenzao Wakenya hawaogopi ndiyo maana waliandamana licha ya wengine kujeruhiwa na kupoteza maisha kwenye vurugu ni mambo ambayo hayana mashiko, kwani inasikitika kwa kilichotokea.
Ikumbukwe kuwa, wanasiasa na wanaharakati wa kisiasa daima wanaangazia maslahi yao binafsi na wanatumia kila fursa, hata kama ni umwagaji wa damu, kutimiza malengo yao ya kusaka uongozi. Kwamba, wataandamana tu hata kama kuna katazo ni uamuzi wa kihuni usiozingatia hali ya amani na usalama wa wananchi wanaoshawishiwa kwa Hila wawe chambo ili wakiguswa tu, basi wao wanasiasa na wanaharakati watapaza sauti zao kwa mabeberu wa kuwatetea.
Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete alipata kusema, akili za kuambiwa changanya na zako. Ni juu ya wananchi wenyewe kupima na kutathmini kabla ya kujihusisha na maandamano hayo, vinginevyo wanaingia kwenye mtego wa wanasiasa wanaotafuta uongozi hata kwa gharama ya damu.
Soma Pia:
Amani na utulivu ni tunu ambazo tunapaswa kuzienzi, na haifai kuvuruga kwa ushawishi wa wachache wenye agenda zao fiche.

- Freeman Mbowe: Tutaandamana kudai watu waliopotea
- Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu