Maandamano ya Jubilee Kuu 2025 jijini Dar es Salaam

Maandamano ya Jubilee Kuu 2025 jijini Dar es Salaam

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
29 December 2024
Dar es Salaam

Maandamano ya Jubilei Jimbo Kuu jijini Dar es Salaam 2025


View: https://m.youtube.com/watch?v=hDK2Hmt-zN8 yaliyoanzia kanisa la St Peters lililopo Oysterbay Mbuyuni hadi kanisa kuu la St Joseph eneo la Posta katika ya jiji la Dar es Salaam eneo la Posta.

Huko Tabora pia Kardinali Protase Rugambwa, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Tabora, Tanzania alisema Tarehe 29 Desemba 2024 ni ufunguzi wa Maadhimisho ya Jubilei kuu ya Miaka 2025 ya Ukristo, tayari kukutana na Kristo Yesu, Lango la Matumaini na Wokovu. Huu ni mwaka wa neema na rehema. Watu wa Mungu Jimbo kuu la Tabora wanaitwa na kutumwa kuwa ni watu wa shukrani katika upendo, imani na matumaini, tayari kumwiga Bikira Maria aliyeshiriki kwa namna ya pekee katika mpango wa Mungu wa kumkomboa mwanadamu.


Kardinali Protase Rugambwa anawaalika watu wa Mungu kushiriki kikamilifu katika mchakato wa ujenzi wa Kanisa kwa nguvu zao na rasilimali walizokirimiwa na Mungu, kwani wanapaswa kuwajibika.


Bikira Maria Mama wa Mungu na Mkombozi wa ulimwengu, awasindikize katika maisha na utume wao. Waamini waweke nia kwa mwaka 2025 ili weweze kufanya mapenzi ya Mungu na waendelee kuombea amani kwa Tanzania, amani kwa Mataifa yote duniani. Mwenyezi Mungu alete amani kule kwenye machafuko, kutoelewana, magomvi na vita. Waamini wamwombe Emanueli, Mfalme wa amani aweke mkono wake na amani yake itawale.
 
Jubilee processions around the world

1735501679619.jpeg
 
Kanisa Moja Takatifu La Mitume😄

John the Batist toa ufafabuzi wa kina tukio hili muhimu kila baada ya miaka 25 yaani Jubilei kwa faida ya wanaJF

Maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei kuu ya huruma ya Mungu ni muda muafaka kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema Jimbo kuu la Dar es Salaam, kusimama, kutafakari na kupiga magoti, ili kila mmoja aweze kutoa mchango wake kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya kanisa la Roma: kiroho na kimwili. Ni changamoto ya kutekeleza wito na wajibu wa kila mtu, ili kujibu kiu ya matumaini ya wananchi walio katika kusanyiko kuu chini ya kanisa moja takatifu kanisa la Roma.
 
Back
Top Bottom