Maandamano ya Jumatano yalazimu polisi kupiga doria nje ya makazi ya Raila Odinga

Maandamano ya Jumatano yalazimu polisi kupiga doria nje ya makazi ya Raila Odinga

Kenyan

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
414
Reaction score
314
Hali ni tete katika maeneo mengi ya Kenya leo baada ya waandamanaji kuitika mwito wa Kiongozi wa Upinzani. Maafisa wa polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji huku idadi ya waandamanaji Leo ikionekana kuongezeka.

Aidha maandamano ya leo yameonekana kuwavutia wananchi waishio kaunti alizopata uungwaji mkono mkubwa Rais Ruto katika uchaguzi Mkuu uliopita. Kwa mfano kaunti mji wa Eldoret ulioko kaunti ya Elgeyo Marakwet umeshuhudia maandamano Leo kwa mara ya kwanza, sawa na mji wa Nanyuki ulioko kaunti ya Nyeri.

Kwa sasa maafisa wa polisi wanapiga doria nje ya MAKAZI ya Raila Odinga katika eneo la Karen japokuwa haijabainika wazi iwapo Odinga alilala nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo.

Swali la msingi wanalouliza washikadau tofauti wa masuala ya uongozi ni Je, Polisi Leo watamkamata Raila Odinga. Ni suala la kusubiri kwa sasa.

Ikumbukwe Odinga anatarajiwa kuhutubia mkutano katika viwanja vya Kamukunji kabla ya kuongoza wafuasi wake kuelekea kati kati ya Jiji.

(Pichani ni waandamanaji katika Jiji la Kisumu, na ya pili Kilifi)View attachment 2685702
 
Back
Top Bottom