Jamani jamani! maandamano ya kuweza kuwastua mafisadi huwa hayapangwi ulizeni kote walikoweza kufanya hiyo kitu. Maandamano huwa yanakuja ghafla kutokana na khali itakayowachukiza wananchi na kuamua kusema basi.
maandamano ya kulindwa na Polisi hayana RAHA...haytatokuwa na tofauti na maandamano ya UWT au Umoja wa Vijana wa CCM.....raha ya Maandamano mpambane na POLISI....na hapo ndipo Ulimwengu utalipuka na kelele zenu...from there we can write a new history...otherwise tuache idea ya Maandamano.
for what i know from JK..Mkiandamana hamtopigwa..mtaachwa ila mtazuiwa tu msifike IKULU au kuleta fujo za kuvunja biashara. JK his heart is soft in nature...Hawezi ona damu ya Mtanzania inamwagwa kwa Maandamano ambayo kesho yake tu watu watasahau....
the way yanavyoratibiwa hapa tayari yashafeli....!!!
Mbona hujabuy idea ya petition mkuu?
Petition ni wazo zuri lakini linakona sana - kwanza kuelewa kwa kina ufisadi, pili kuwa na muhutasiri mzima wa hatua zilizochukuliwa, tatu ufafanuzi wa athari zilizopo kwa hatua zinazochukuliwa, nne mapendekezo ya nini kifanyike, na mwisho msimama! kama unauwezo, weka hoja chini na msimamo utakao wakilisha wananchi. Itume hapa gulioni kwanza wenye information waifanyie kazi!
YAP PETU HAPA,
Wazo zuri la uzalendo.
O.K lets go ahead. Tusichelewe tuanze kuongea na kupanda kabla hili vuguvugu halijapoa.
tatizo ni kuwa kila mtu yuko bize kutatua shida zake za kimasikini kila siku, hivyo tukiacha ikipoa basi tena.
Kama kuna mchango sema
Kina Zitto na kina Slaa na kina mama Kilango na kina Selelii.. ndio walitakiwa kuonekana mitaani na mabango wakiongoza maandamano dhidi ya ufisadi na wakiwa na ajenga zilizo wazi:
a. Rostam ajiuzulu
b. Mashtaka ya EPA yawe ya kuhujumu uchumi
c. Chenge ajiuzulu
d. Mramba ajiuzulu
e. Kiwira irudishwe kwa wananchi
f. Benki Kuu ichunguziwe na chombo huru
g. Peter Noni aunganishwe na wenzake kwenye kesi
h. DPP afanye kazi aliyoapishwa kuifanya vinginevyo ajiuzulu
i. Mapendekezo yote ya Kamati Teule yafanyiwe kazi!
Ni maandamamano hayo ambayo yana malengo yaliyokuwa wazi, politically provocative ndiyo yanaweza kugusa watu.... ila sijui kama Lipumba atakuwa tayari kuungana nao!
Kina Zitto na kina Slaa na kina mama Kilango na kina Selelii.. ndio walitakiwa kuonekana mitaani na mabango wakiongoza maandamano dhidi ya ufisadi na wakiwa na ajenga zilizo wazi:
a. Rostam ajiuzulu
c. Chenge ajiuzulu
Ni maandamamano hayo ambayo yana malengo yaliyokuwa wazi, politically provocative ndiyo yanaweza kugusa watu.... ila sijui kama Lipumba atakuwa tayari kuungana nao!
Nguvu ya kuwalazimisha wabunge kujiuzulu ipo kwa umma wote wa tanzania, ama ni wananchi wa jimbo husika? Taratibu zake zikoje?
Sina wasiwasi na lipumba! I will be worried more with Mama Kilango na Seleli - kwa sababu kwa njia moja ama nyingine watakuwa wanasema serikali iwajibike. I am sure of their political stand on Ufisadi, but i am not sure in their stand activism politics out of parliament!