Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wanawake hao, baadhi wakiwa na vifua wazi, na mabango, walikamatwa walipokuwa wakielekea Bungeni huku wakipiga kelele za kupinga ufisadi na serikali.
Waandamanaji hao wametambulika kama Praise Aloikin, mwanafunzi wa sheria katika Chuo Kikuu cha Makerere, Norah Tshetshe, na Kemitoma Siperia Mollie, kiongozi wa zamani wa serikali ya wanafunzi.
Kwa mujibu wa Luke Owoyesigyire, ambaye ni Msemaji wa Polisi, amesema watatu hao wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (CPS) Kampala kwa mashtaka ya kusababisha usumbufu.