Ni matokeonya kufanya kazi kwa propaganda. Serikali imeacha ukweli limekuwa jukwaa la uzushi na majungu na haya ndiyo matokeo.
Tulikuwa na Edward Moringe Sokoine, peke yake Tanzania ilitetemeka na aliweza kusimamia maelekezo yake vema na kwa ufanisi
Tukampata Augustine Lyatonga Mrema kama sokoine nchi ilitulia wezi, vibaka na wabakaji walitulia maana jamaa alifanya kazi
Leo hii, pamoja na maendeleo ya sayansi na technolojia, mambo ndiyo yanazidi kuharibika kila leo afazari ya jana.
Siasa safi imeporomoka imekuwa siasa chafu ya akina mwigulu, Nape na wasira majungu, uzushi na mipasho wala hawakemewi
Afya na elimu bora imekuwa kwa watu wachache wenyefedha na zaidi mafisadi, sehemu kubwa ya watanzania imebaki kutaabika
Usalama na haki kwa watanzania imebaki kwa wenyefedha na mafisadi, masikini, wakinamama, watoto na wanafunzi ni wahanga wa ubakaji na unyang'anyi.
Polisi imebaki kuwa kikundi cha wahuni wa kuitumikia ccm na mafisadi, wameacha misingi ya uwajibikaji kutoka katiba nasasa sio walinzi wa usalama wa raia na mali zao bali wamegeuka kuwa walinzi ccm na malengo yake ya kifisadi.
Katika yote hayo
Kikwete yupo madarakani anachokifanya anakijuwa yeye na inawezekana anafahamam vema malengo ya wahuni hawa.
1. makanisa yamechomwa tena mengi, rais amekaa kimya haiwezekana kwa idadi kubwa kiasi kile asifahamike mchomaji.
2. Askari wake wamemuuwa mwangosi, kikwete kashindwa kumuadhibu kamuhanda anataka ushahidi gani zaidi ya ule?
3. Mwanahalisi katoa habari za kiuchunguzi kuhusiana na mtesi wa Ulimboka, cha ajabu anafungiwa badala ya kumwita awasaidie.
4. Askari polisi wameuwa Songea, morogoro, Arusha nk, kikwete katia pamba masikioni na kuvaa miwani ya mbao
5. Polisi wamekwapuwa mamilioni Dsm, kova kakiri hatua zilizochukuliwa zipo kwenye mabano haijulikani nani kaadhibiwa
Kunamambo mengi sana yanayopingana na utawala bora na uwezo wa Kikwete katika kuiendesha nchi, matokeo yake wahuni
sasa wameingia hadi vyuoni sio wanaiba tu bali wanabaka na kuuwa wanafunzi tena sio chuo kimoja na wala sio mara moja ni
mara kadhaa.
Wenye hekima wanajiuliza
-waziri wa ulinzi yupo wapi?
-Said mwema yupo wapi?
-Kova na mbwembwe zake yupo wapi?
-Manumba yeye yuko ICU lakini alikuwa wapi siku zote?
Mwisho Rais yupo wapi kwanini hawawajibishi hawa watendaji wake kwa kushindwa kuwalinda watanzania? kwakukaa kimya
kikwete bila kuwaadhibu watendaji wake ndipo napata mashaka kwamba inawezekana akawa nyuma ya mpango mzima.