Maandamano yaibuka Syria kufuatia kuchomwa kwa mti wa Krismasi

Maandamano yaibuka Syria kufuatia kuchomwa kwa mti wa Krismasi

Narumu kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
1,888
Reaction score
4,489
Maandamano yameibuka nchini Syria kufuatia kuchomwa kwa mti wa Krismasi karibu na jiji la Hama.

Video iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha wapiganaji waliovaa barakoa wakichoma mti ulioonyeshwa kwenye uwanja mkuu wa Suqaylabiyah, mji unaoongozwa na Wakristo katikati ya Syria.

Kundi kuu la Kiislamu linaloongoza mapinduzi yaliyomuondoa Rais Bashar al-Assad limesema kwamba watu waliotekeleza tukio la kuchoma mti ni wapiganaji wa kigeni na tayari wametiwa nguvuni.

Maelfu ya waandamanaji walijitokeza mitaani kote nchini, wakiitaka serikali mpya ya Kiislamu kulinda haki za wachache wa kidini.

Picha za tukio hilo zilionyesha kiongozi wa kidini kutoka kwa kundi la waasi la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) akiwahakikishia watu waliojitokeza Suqaylabiyah kuwa mti huo utarekebishwa kabla ya asubuhi. Kiongozi huyo alionyesha msalaba kama ishara ya mshikamano, jambo ambalo wahafidhina wa Kiislamu wangeepuka kufanya.

Katika eneo la Bab Touma la Damascus, waandamanaji walibeba msalaba na bendera za Syria, wakisema “Tutatoa roho zetu kwa ajili ya msalaba wetu”.

“Mambo ikiwa hayaturuhusu kuishi imani yetu ya Kikristo nchini mwetu, kama tulivyokuwa tukiishi zamani, basi hatustahili kuwa hapa tena,” alisema mtetezi mmoja aitwaye Georges kwa shirika la habari la AFP.

Syria ina makundi mengi ya kikabila na kidini, ikiwa ni pamoja na Wakurdi, Waarmenia, Waashuru, Wakristo, Druz, Waislamu wa Kishia wa Alawite na Waislamu wa Sunni, ambao ni wengi kati ya Waislamu.

Viongozi wa HTS walizungumza kuhusu kujenga Syria kwa ajili ya Wasyiria wote, na kusema kwamba haki na uhuru wa wachache wa kidini na kikabila watalindwa.

Ijumaa, Marekani iliondoa dau la $10 milioni kwa mkuu wa HTS, Ahmed al-Sharaa, baada ya mazungumzo kati ya mabalozi wa juu na wawakilishi wa kundi hilo.

Marekani inaendelea na uwepo wake wa kijeshi Syria. Imetangaza Ijumaa kwamba ilifanya shambulio la angani katika mji wa kaskazini wa Deir Ezzor, na kuua wanachama wawili wa kundi la jihadi la Islamic State (IS).

Uwepo wa wapiganaji wa kigeni, wanaharakati wa Kiislamu, au hata wafuasi wa utawala ambao wanavutiwa na kuleta usalama na kushambulia wachache ni changamoto kubwa ambayo uongozi mpya wa Kiislamu utakuwa nayo.
 
Hatimaye Syria imekombolewa kutoka katika makucha na makanywa ya mbweha wa jangwani! Mungu wa Mbinguni awabariki sana!
 
Hatimaye Syria imekombolewa kutoka katika makucha na makanywa ya mbweha wa jangwani! Mungu wa Mbinguni awabariki sana!
Katika kundi lililo kuwa linaishi vizuri na kwa uhuru chini ya utawala wa Asad ni wakristo.
Asad si mtu aliye kuwa ana amini kwenye uongozi wa kidini, lakini walio chukua madaraka kwa sasa ni makundi ya kiislam tena ya kisuni kwa sasa bado ile furaha ya kupata madaraka bila kutarajia bado ipo kichwani ,sasa subiri walewe madaraka mtaona sura zao halisi.
 
Let's wait and see.
 
Syria 🇸🇾 is no longer at ease.
Kobazi kuachiwa nchi cha moto watakiona.
 
Back
Top Bottom