Maandamano yaingia usiku karibu na majengo ya Bunge, Nairobi (video)

Maandamano yaingia usiku karibu na majengo ya Bunge, Nairobi (video)

Ikaria

Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
93
Reaction score
238


Waandamanaji wanaendelea kuandamana kwa kuwasha moto katika Barabara ya kuelekea mzunguko wa Holy Basilica, karibu na Majengo ya Bunge.

Licha ya maandamano ya mchana kutwa, Wabunge 204 wamepiga kura kupitisha mswada huo, huku Wabunge 115 wakipiga kura kuupinga.

Hatua ipi inafuata sasa kuhusu mswada huo tata?

✓ Hatua inayofuata ni Kamati ya Bunge lote, ambapo marekebisho kwenye mswada yatapendekezwa na vipengele vya mswada kupigiwa kura, na kufanyiwa nyongeza endapo itahitajika.

✓ Hii ni hatua muhimu ya kufuta, kubadilisha au kutunza baadhi ya vipengele vya mswada huo.

Mambo muhimu kufahamu kuhusu maandamano haya dhidi ya serikali:

1. Hii ni mara ya kwanza Wakenya kuandamana dhidi ya Serikali bila ya kuchochewa na Mwanasiasa Wala chama chochote cha kisiasa.
2. Idadi kubwa ya waandamanaji ni vijana husan kizazi cha GenZ.
3. Waandamanaji hawakupora Mali Wala kutupa mawe mchana kutwa.
4. Kuna hofu huenda watu wenye nia mbaya wakapora Mali ya watu, maadamano yakiendelea usiku kucha.
---
Maandamano ya kupinga mapendekezo ya ongezeko la kodi katika Muswada wa Fedha wa 2024/ 2025 nchini Kenya yameingia siku ya pili, huku kukishuhudiwa matukio ya watu kuumia kutokana na ghasia hizo.

Mamia ya wananchi wamejitokeza katika kaunti za Nairobi, Kisumu, Kakamega, Eldoret, Kilifi, Nakuru, Nyeri, Nanyuki, Embu kuandamana leo Juni 20, 2024 ikiwa ni siku ya pili wakipinga Muswada wa Fedha kwa mwaka wa fedha 2024/ 2025.

Aidha, wananchi hao wameingia barabarani wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti tofauti kupinga ongezeko hilo la kodi lililowasilishwa bungeni Jumanne Juni 18, 2024 kwa ajili ya kuanza kutumika kwa mwaka wa fedha 2024/ 2025.

Polisi nchini humo wanapambana kuwatuliza raia hao wanaoonekana kuwa na hasira kali wakitumia mabpmu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha ili kuwatawanya lakini wameonekana kutokubali kuondoka barabarani kwa siku ya pili leo.

Maandamano hayo yamepelekea baadhi ya raia na maofisa wa polisi kujeruhiwa na hata wengine kupata ulemavu akiwemo ofisa wa Polisi, David Maina ambaye amepoteza mikono yote miwili baada ya bomu la machozi kulipuka wakati wa maandamano.

Pia, katika Jiji la Nairobi baadhi ya mawakili wamejitokeza kuungana na wananchi hao kuendelea kupinga ongezeko hilo na kodi huku Bunge likiendelea na vikao vyake.

Kilio kikubwa cha wananchi wa Kenya ni ongezeko kubwa la kodi linalowapelekea kuwa na mzigo mkubwa unaowasababishia ugumu wa maisha.
 
Back
Top Bottom