Hayo maandamano hayatawezekana kwasababu zifuatazo
1-Hatuna umoja. Wakati wewe unaona uchungu nchi kuwa gizani na kukosa maji, upande wa pili kuna maelfu ya vijana (chaws) wapo tayari kutetea upuuzi wawanaoitwa viongozi kwa ujira wa vipesa vidogo tu.
2-Maandamano hayaonyeshi wazi nini hasa kitafanikiwa baada ya hayo maandamano? Au ndiyo kuandamana tu? Halafu ikifika jioni unarudi nyumbani? Sasa tutakuwa tumefanikiwa nini hapa?
3-Maandamano kuwa na itikadi za kichama badala ya ajenda zinazolenga kutatua kweli changamoto zetu wadanganyika. Na hii inaturudisha kwenye point namba moja, tunagawanyika. Ujinga mtupu.
4-Watu wanaoguswa na tatizo la ukosefu wa umeme na maji na kweli wanasikia maumivu ni idadi chache tu yawatanzania. Idadi kubwa ya watu hawana kazi zinazohitaji umeme kwahiyo hawawezi kuona umuhimu sana.
Watanzania watakuwa tayari kudai maendeleo yenye tija mpaka siku ile…ile siku.
Wanasiasa watakapoanza kushika wananchi makalio.