Maandamano ya DP World - Bandari yalishika kasi zaidi Mbeya, Kesi ilifunguliwa Mahakama ya Mbeya
2011 kulikuwa na Maandamano ya Machinga, Askari wa FFU baadhi waliuawa na mabomu ya machozi yaliisha, Muda huo Kikwete yupo njiani kuelekea Mbeya, Ilibidi watumwe JWTZ kutuliza hali (hakukuwa na majibishano yoyote na JWTZ)
Kwenye maandamano mengine ya Machinga, hali ilikuwa mbaya, Mkuu wa mkoa wa enzi hizo Abas Kandoro alikimbilia uwanja wa ndege.
Huko Chunya enzi za Kikwete alienda kuhutubia, Wananchi wakamuuliza unaenda sana nchi za nje wakati huku kwetu hali mbaya inakuwaje hii, Tafrani ikazuka Rais akawahishwa kwenye gari, wananchi wakaziba njia na kuanza kuipiga gari mawe, Ni umahiri wa dereva ndio ulioweza kusaidia kuondoka kwenye eneo haraka