Maandamano yanaendelea Kenya muda huu, mtu mmoja auawa

Maandamano yanaendelea Kenya muda huu, mtu mmoja auawa

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
559
Reaction score
808
160606100752_kisumu_demo_512x288_bbc_nocredit.jpg

Waandamanaji wa upinzani nchini Kenya wamefunga barabara kwa kuchoma magurudumu katika mji wa Kisumu ulio magharibi mwa nchi hiyo.

Waandamanaji hao wanataka tume ya uchaguzi nchini Kenya kufanyiwa mabadiliko.

Ghasia hizo zinashuhudiwa licha ya mkuu wa polisi katika mji wa Kisumu kuwaonya watu na kuwataka wasishiriki maandamano hayo.

Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa mtu mmoja ameuawa wakati wa maandamano ya mji wa Kisumu
 
hahaha hv uhuru kenyatta kipindi hajawa rais si aliwahi kuilalamikia tume ya uchaguzi na yy anafanya yaleyale aliyokuwa anayalalamikia. hahaha kwl afrika ni miyeyusho.
 
yaani wakenya wana katiba mpya lkn malalamiko kila siku, wanataka kutuambia katiba mpya sio dawa ya matatzo katka serikali.
 
Wakenya wanajua kupigania haki zao.

Wametaka kuandamana. Polisi wamewakataza kuandamana kwa sababu ya ujinga wa kibali. Wameenda mahakamani kushitaki na kushinda kesi. Polisi wameamriwa na mahakama kutoa ulinzi.
 
yaani wakenya wana katiba mpya lkn malalamiko kila siku, wanataka kutuambia katiba mpya sio dawa ya matatzo katka serikali.
Hiyo Katiba Mpya ndo inawasaidia kuweza ona mapungufu ya Tume la Uchaguzi na Mipaka. Bila Katiba Mpya ingeokena kila kitu iko sawa.
 
mimi naona haya mambo ya kuandamana na kwa ajili ya wanasiasa hayana tija , mnaishia kupoteza wote tu...Kenya achaneni na maandamano yataleta machafuko, fanyeni kazi ndio msingi wa maendeleo
 
yaani wakenya wana katiba mpya lkn malalamiko kila siku, wanataka kutuambia katiba mpya sio dawa ya matatzo katka serikali.
Kaliaga kuwabeza huku wenzio wameshafikia mawazo na ujasiri wa kuikataa tume ya uchaguzi, wewe naamini hujui hata makao yake yalipo!
Na katika ubishi wao huu unawawezesha hadi sasa kuwa nchi pekee iliyokamilisha ada zake za EAC. Wenzetu wanaenda mbele sisi hata njia hatujui iliko.
 
Kenya siku hizi limekuwa ni Taifa la maandamano.
 
Ngoja waandamane wadai wanachokitaka, sijui kwanini huku Africa watu wakiandamana lazima vifo vitokee? Hapa kuna walakini, waandamanaji na polisi wote wanakuwa na munkari
 
mimi naona haya mambo ya kuandamana na kwa ajili ya wanasiasa hayana tija , mnaishia kupoteza wote tu...Kenya achaneni na maandamano yataleta machafuko, fanyeni kazi ndio msingi wa maendeleo

Acha uoga
 
Haki huwa haiombwi bali inadaiwa na maandamano ndio njia pekee ya kudai haki...!ila hawa polisi wa Kenya wamezidi ubabe naona hawatambui kazi yao!
 
Wakenya wanajua kupigania haki zao.

Wametaka kuandamana. Polisi wamewakataza kuandamana kwa sababu ya ujinga wa kibali. Wameenda mahakamani kushitaki na kushinda kesi. Polisi wameamriwa na mahakama kutoa ulinzi.
Hapa kwetu sijui kwa sasa kama hilo la kutumia mahakama kupata haki kama litawezekana.
Bunge kama mhimili unaojitegemea tunaona unaingiliwa na serikali, sasa kama wameweza kuingilia Bunge, watashindwa ilazimisha mahakama kupinda pinda?
 
Kaliaga kuwabeza huku wenzio wameshafikia mawazo na ujasiri wa kuikataa tume ya uchaguzi, wewe naamini hujui hata makao yake yalipo!
Na katika ubishi wao huu unawawezesha hadi sasa kuwa nchi pekee iliyokamilisha ada zake za EAC. Wenzetu wanaenda mbele sisi hata njia hatujui iliko.
ukondoo ndio unawaponza wa Tanzania, ubishi nao unawaponza wa Kenya
 
Back
Top Bottom