Maandamano yanayoambatana na kuharibu mali kwa kisingizio cha Demokrasia

Maandamano yanayoambatana na kuharibu mali kwa kisingizio cha Demokrasia

Maria Nyedetse

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2021
Posts
661
Reaction score
1,501
Naomba kabla sijaendelea kusema jambo moja... "Naunga mkono vuguvugu za kidemokrasia ambazo sii za vurugu" Daima siungi mkono vurugu kwa kisingizio cha Demokrasia.

Wanajamvi leo naomba kusema kitu ambacho najua wengi wetu wanaweza wasinielewe LAKINI naamini kuna watakaonielewa.

Mara nyingi kuna watu hutumia hisia zetu za kupata uhuru wa kidemokrasia kwa ajili ya kupata miradi yao ya kisiasa au hata kwa kutumiwa wa wenye maslahi kutoka nje ya nchi husika kwa wao kupata vipande vya fedha.

Ndugu zangu ukiangalia YEMENI, SOMALIA, SYRIA, LIBYA na kwingineko baadhi ya watu walitumika kuamsha vuguvugu za kudai Demokrasia lakini kwa njia ya KUTUMIA NGUVU au VURUGU... mara nyingi vitendo hivi hutoa nafasi kwa wenye nia zingine ovu huingilia kati na mambo huenda holijojo.

Na hali ikifikia hapo mamilioni hupoteza maisha, uwezo wa kuendesha maisha yao ya kila siku, ulemavu wa kudumu, kutengana kwa familia, watoto wa mitaani na umasikini uliokithiri.

Hapa ile "social order" huondoka na mambo mengi maovu huibuka ikiwemo utumikishaji wa watu, usafirishaji Haramu wa binadamu na biashara haramu ya viungo vya binadamu kama figo, moyo na mfano wake... wengi huteseka na kudhalilika.

Ndugu zangu daima huwa namkubali sana Mahatma Gandhi kwa njia yake ya "non violence" kwa viwango hivi vya kawaida vya udhalimu wa viongozi wetu wengi kama walivyo viongozi wa kiafrika daima sii busara kuanzisha "violent demonstrations" kwa sababu ni rahisi to get out of control na hali kuwa mbaya na kukosa wa kuidhibiti.

Mara nyingi wanasiasa hushawishi njia hii kwa sababu malengo yao ni ya muda mfupi wa kupata madaraka na kamwe hawana malengo ya muda mrefu ndiyo maana kwao as long as anaweza kupata anachotaka basi kwake kushawishi kutumika nguvu wala haoni shida lakini bila kujali maisha ya watu wangapi yataharibika.

Leo Nchi nilizotangulia kuzitaja hapo kama wangepewa fursa ya kuchagua unafikiri wangechagu NINI? mara nyingi tukila tukashiba, tuna familia zetu na tuna pakulaza mbavu zetu huwa tunadanganyika lakini uhalisia huwa tunaghilibiwa na wachache.

Ni bora kuwa na kiongozi dhalimu kiasi kuliko kukosa kiongozi na nchi kuparaganyika.

Leo ndugu zetu wasomalia kila siku wanakamatwa wakiingia nchini kuelekea Afrika kusini sii kwamba wanapenda ila ni kutokana na hali ngumu nyumbani na wakati mwingine hufia kwenye maloria wakipakiwa kama mizigo kukwepa vyombo vya dola.

WITO WANGU... wakati wote tudai Demokrasia zetu kwa njia ya amani na majadiliano na njia zingine zisizo za VURUGU kama mgomo wa kula na mfano wake.

Tusitumike kufanya mambo ambayo hatui uhakika wa kesho yake.

Leo Yemeni, Syria, Libya ni zaidi ya miaka 10, na SOMALIA ni zaidi ya miaka 30. waliambiwa Siad Bare ni dikteta na wakatumainishwa nchi ya ahadi kwa kumtoa na wakakubali matokeo yake wametokea JEHANAMU badala ya EDENI.... SO SAD

TUAMKE NA TUTUMIE AKILI BADALA YA KUTUMIA HISIA.

Ni mawazo na Mtazamo binafsi, tujadiliane kwa hoja bila matusi wala mihemko... huna hoja bora kusoma comments na sii kutoa MAPOVU
 
Back
Top Bottom