Maandiko haya yalikuwa na maana gani? Au yalikuwa yanawahusu wakina nani?

Maandiko haya yalikuwa na maana gani? Au yalikuwa yanawahusu wakina nani?

The master

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
289
Reaction score
195
Amani iwe kwenu nyote.

Biblia ni kitabu ambacho kimeeleza maisha ya mwanadamu tangu kuumbwa kwa dunia hadi ukamilifu wa dahari. Japokuwa kina aya nyingi zinazokinzana lakini wasomi wengi wa mambo ya dini wanakitumia kitabu hicho kama rejea ya mambo mbalimbali ya kiimani. Nirejee kwenye mada.

Mada yangu inahuru Mathayo 21:33-44. Kwa wale wasoma biblia watatambua kuwa Yesu alitoa mfano wa mtu mmoja aliyelima shamba la mizabibu kisha akaenda mbali.

Lengo langu hapa si kuleta ubishani wa kidini bali ni kuelimishana kwa lengo la kujifunza. Biblia inasema kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na hivyo mshike sana elimu usimwache aende zake. Pia inasema tuitafute kweli kwani kweli itatufanya kuwa huru.

Karibuni tuelimishane kwa ushahidi na si kukejeliana.
 
Mkuu hapa Yesu analizungumzia Taifa la Israel ambalo Mwenyezi Mungu aliliteua na kisha kuwapa nchi ya Ahadi iliyojaa Maziwa na Asali,Mungu akawatuma Manabii ili kuwaongoza watu namna sahihi ya kumtumikia Mungu lkn Waisraeli waliwaua hao Manabii(Mt 23:37),Ndipo baadaye Mwenyezi Mungu akaamua kumtuma Yesu Mwanae wa Pekee ili kuukomboa Ulimwengu lkn bado Waisraeli haohao Wakamuua;Ktk mfano huu Mtu mwenye nyumba ni Mungu Mwenyewe,Shamba la Mizabibu ni Zawadi ya Mungu kuwa mteule wake kati ya Mataifa(aliyokuwa amepewa Israel),Wakulima hao ni Wana wa Israeli,Watumwa ni Manabii waliokuwa wametumwa na Mungu ktkt Taifa la Israeli,Mwana wa Mkulima ni Yesu Kristo,Matunda ni Matokeo chanya yanayopatikana kutokana na namna Mwanadamu anavyoishi na kujitoa ktk kumtimikia Mungu,Kuwafukuza hao wakulima na kuwapangisha wengine m.y.ni kwamba Mungu atalipokonya Taifa la Israeli kuwa taifa teule na kisha kuwashirikisha hata Mataifa mengine zawadi hiyo aliyokuwa amepewa Israel.
 
siku ya mwisho waafrika hatutahukumiwa dini waliletewa waarabu
 
Samahanini kwa kuchomeka swali juu ya swali ila naomba mwenye tafsiri ya yale maandiko katika kitabu cha Luka 20:17
 
CHAULA RICH

Kwahiyo Taifa la Israel si taifa teule tena la Mungu? Na kama siyo je alipo sema atawapa wengine alimaanisha wakina nani? My take kuwapa wengine si kwamba kila mtu atakuwa huru kulitunza shamba hilo. Hivyo kwa maoni yangu kuna taifa lingine litakalokaabidhiwa kulitunza shamba hilo. Sijui kama nitakuwa nakosea na kama kuna taifa lingine ni taifa gani hilo?
 
Mkuu Mungu sasa ameyafanya Mataifa yote kuwa warithi wa Ufalme wake Mathayo 28:19;Yohane 1:12.
 
mfumo bora wa maisha kwa binadamu ni ubepari wenye kusimamia unyonyaji kwa wanyonge. those who are reach are blessed and curse to those who are poor and slaves
 
CHAULA RICH

Kwahiyo Taifa la Israel si taifa teule tena la Mungu? Na kama siyo je alipo sema atawapa wengine alimaanisha wakina nani? My take kuwapa wengine si kwamba kila mtu atakuwa huru kulitunza shamba hilo. Hivyo kwa maoni yangu kuna taifa lingine litakalokaabidhiwa kulitunza shamba hilo. Sijui kama nitakuwa nakosea na kama kuna taifa lingine ni taifa gani hilo?

yap, na taifa hilo si lingine bali ni tanzania (gosheni), ambapo Injili ya kanisa la mwisho imeanzia, na sasa inaenea kwa kasi Africa na ulaya.
 
Back
Top Bottom