Maasai vs Mchaga

Maasai vs Mchaga

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Msonjo amenunua gari kwa ajili ya biashara ya daladala, ameenda kuomba leseni ya usafirishaji abiria. Ikawa hivi:-

Msonjo – wewe mama, mupe mimi laseni (leseni) ya gari.

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – leseni ya udereva au? Gari ya kazi gani?

Msonjo – wewe hapana sikia musuri? Asisumbue mimi!

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – Masai, kwa upande wa vyombo vya usafiri kuna leseni ya udereva na biashara, umeelewa?

Msonjo – kabisa, mupe hiyo dereba na biashara.

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – kwahiyo unataka leseni mbili au?

Msonjo – mbona wewe anasumbua sana? Wewe anasema iko laseni ya dereba na biashara, sasa anaulisaje tena laseni mbili? Si wewe anasema iko ya dereba na biashara, mimi anamwambia mupe hiyo moja ya dereba na biashara, sasa anaulisa laseni mbili tena?! Eih!… Ng’arrryagalagalong’! Lagabarayaiya!

Mlinzi wa Ofisi (Murimi Magabe) – anaingilia kati baada ya kuona mori unapanda. Anatoa ufafanuzi mzuri kwamba wewe Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) umemwambia Yero kuna leseni ya udereva na biashara, sasa yeye ameelewa kwamba leseni moja hiyo inafanyakazi mbili za udereva na biashara. Ulitakiwa umwambie kwamba kuna leseni moja ya udereva na leseni nyingine ya biashara ili achague.

Msonjo – kabisa… kabisa…, wewe Polisi iko akili mingi kabisa, mimi atamupa wewe ndito yangu.

Wateja– wakaangusha kicheko hahahahaaa…

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – nisamehe Masai. Sijui nikupe leseni ipi sasa?

Msonjo – mimi hapana dereba.

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – kwahiyo nikupe ya biashara.

Msonjo – kabisa.

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – biashara gani, ya kusafirisha mizigo au abiria?

Msonjo – watu, aribia ni watu? Anamuuliza Afisa-Leseni Nkyekuu Minja.

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – ananigwa na kicheko na kujibu: ndiyo, abiria ni watu.

Msonjo – kabisa.

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – njia gani unachagua?

Msonjo – kimya… makengeza kodo, hajaelewa swali. Anauliza, si huyu njia anakaa kwa udongo (akimaanisha barabara).

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – (kuogopa mori kupanda tena) safari hii kajipanga kufafanua vizuri: ninamaanisha gari yako itabeba abiria toka wapi kwenda wapi? Yaani ruti.

Msonjo – Saredalaam (Dsm) mupaka Sansibaa (Zanzibar).

Wateja – hahahahaaa… hahahahaaa… uuuwiiiii…, sinema tamu hii kwelikweli, bora iendelee bila kukoma hahahahaaa… jamani! Duh! Hii kali ya mwaka.

Msonjo – mori ukapanda upya, anacheka nini nyie? Anacheka nini? Sansibaa hayuko Tansania? Ikabidi wateja watulizwe.

Mteja mmoja – akadakia: Masai, kuna bahari kwenda Zanzibar, gari yako itapitaje kwenye maji?

Msonjo – wacha urongo wewe…, anasoma ngapi wewe! Kama Sansibaa angekuwa ana maji (bahari) Makufuli angejengaje parapara ya Tansanait toka Saredalaam mupaka Sansibaa? Angejenga namuna gani parapara bayarini (baharini)? Wacha umbeya…

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – akaibuka toka chini ya dawati alipojificha kucheka na kusema: Dar es Salaam kwenda Zanzibar hatuna njia hiyo kwa vyombo vya moto vya usafiri wa nchi kavu!

Msonjo – Mbona Apolo ya Mirerani anamwambia mimi Saredalaam mupaka Sansibaa ana ela mingi alafu panya hapana kukula parapara (mashimo).

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – gari yako ni aina gani? Ngoja kwanza tujuwe aina ya gari.

Msonjo – ile mupya ya sasa.

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – mpya ya sasa?! Ikoje hiyo! Umekuja nayo?

Msonjo – kabisa.

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – Mlinzi nenda naye ukaiangalie ni aina gani.

Mlinzi (Murimi Magabe) – anarudi amepaliwa na kunigwa kicheko kwa siri.

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – gari gani hiyo?

Mlinzi (Murimi Magabe) – Kirikuu ya namba AAA.

Afisa-Leseni (Nkyekuu Minja) – uuuwiii... jamani, mimi leo nafanyaje huyu mteja? Kichwa kinauma… ee Mungu nisaidie…

Wateja – wakalipuka tena kicheko hahahahaaa… hahahahaaa… waaayiii…. jamani kumbe kabila langu zuri eee…, baadhi wanasema: huyo anataka leseni ya abiria toka Dar es Salaam kwenda Zanzibar ili akachukuwe abiria akawape Nyangumi na Papa kama kafara ili biashara yake ya madini impe ela nyingi, hawa ndivyo walivyo, wakiona biashara yao ya madini inazorota tu wanaanza kuwafaidisha waganga wa kienyeji.

Afisa-Leseni mwingine (Nkansee Swai) – hawa watu wagumu sana, inabidi kuwa nao makini sana. Kuna mmoja aliwahi kuja kuomba leseni ya abiria baada ya kupata ela zake za madini huko kwao. Aliomba leseni ya Kariakoo Mbagala enzi za magari aina ya Hiace, tunakuja kupewa taarifa ya leseni zilizofutwa kwamba kosa lake lilikuwa ni kutumia leseni ya abiria Kariakoo Mbagala kusafirishia maziwa toka Chalinze kwenda Kariakoo, yaani akavuka nje ya mkoa wa Dsm.

Tukio siyo halisi.
 
Back
Top Bottom