Maazimio mangapi ya mwaka mpya umeshayavunja?

Maazimio mangapi ya mwaka mpya umeshayavunja?

Execute

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
3,000
Reaction score
7,336
Kuna maazimio mazito niliyaweka lakini wapi nishapoteza mengi tu. Nilisema sitakunywa soda na nimeshakunywa tano, nilisema sitatumia sukari na nishainywa.

Nilisema sigusi nje tayari kuna mmoja alijileta. Yaani tafrani tupu.
 
Nashukuru Mungu sijafanya zinaa toka mwaka uanze. Mungu ajaalie niendelee hivyo hivyo.

Nililipia gym ili nianze tizi la kupungua na kuahidi kuanza kula kiafya.
Gym nimeenda siku moja tu, tarehe moja January. Tumbo limejaa ndi hapa nilipo kwa ubwabwa, maharage ya nazi, kuku wa kukaanga na lita moja ya juisi ya miwa.
Mungu nisaidie.
 
Kuna jamaa alisema ameacha pombe lakini juz kaja amelewa kazini, ukimuuliza nn tatizo na ulisema umeacha pombe mwaka uliopita anabaki kucheka, anasema hata yeye hajui nini tatizo
Kuna watu watasema huyo jamaa ndio wewe
 
I plan according to context not according to new year
 
Nimeazimiq kuanzia mwaka huu kuishi miaka 120 nikiwa na nguvu. Sasa niko kwenye reverse process ya kula anti aging foods kioaumbele kikiwa ni matunda nafaka na mbogamboga.
Na nasoma lifestyle ya maeneo ambayo watu wanatoboa 100 bila nguvu huku nikiwakimbia watu hasi. Hadi sasa naenda vizuri ila kuna misimamo niliyojiwekea mingine bado haijastabikize najikuta naanguka ila sirudi nyumq. Kwa sasa nimeweka plan ya miaka 25 ya kwanza.
 
Mimi huu mwaka niliamua kabisa kua mwaka wangu utaanza tarehe 1 mwezi wa nne.
Kwaio tukutane huko.
 
Kwa ufupi ni kuwa wote mlioshindwa kusimamia malengo yenu ni mnakosa self-discipline.
 
Moja ya maazimio makubwa ambayo watu huweka ni mazoezi/kupunguza uzito lkn mpaka sasa wengi washaacha hayo mazoezi uchwara[emoji23][emoji23]
Mi naanzaga kwa fujo kama.wiki tatu hivi halafu ntakavyoacha hata sitajua nimeachaje na nina gym nyumban
 
Back
Top Bottom